Mwinjilist mtume nabii
JF-Expert Member
- Feb 21, 2015
- 2,437
- 1,097
Mkuu Illovo,jazia habari yako tukusaidie. Mkataba gani unaouzungumzia? Hapo Kiwandani kuna vyama vingapi vya wafanyakazi?
Mkuu Kimoja Ndo Kilikuwepo Cha TPAWU, lkn sasa kuna TUICO nao wanataka kuingia na watu tayari wamejaza fomu za kujiunga, tafadhali msaada plz, mm ndiye reporter wa ukweli
Mkuu Illovo,jazia habari yako tukusaidie. Mkataba gani unaouzungumzia? Hapo Kiwandani kuna vyama vingapi vya wafanyakazi?
Eti Ule Mkataba Wa Hiari Yaan "CBA" Collective Bargaining Agreement, utafutwa kwa kuwa chama cha kwanza ndo kilikubaliana na mwajiri
CBA husainiwa na Chama cha Wafanyakazi pamoja na Mwajiri. Chama hicho cha wafanyakazi lazima kiwe kile chenye wanachama wengi kuliko kingine kama kipo. Kisheria,mfanyakazi ana hakya kujiunga na kujitoa toka chama chochote cha wafanyakazi. TPWU itabaki kwenye CBA hadi pale kitakapozidiwa na kingine katika idadi ya wanachama.
Naiona kauli ya TPWU kama mkwara tu kuzuia kukimbiwa. TUICO ianzishwe na wanachama wajiunge na kujitoa katika chama chochote. Anza na hayo Mkuu Illovo
Sawa Mkuu, Sasa Ikitokea TUICO ikawa na watu wengi kuliko TPAWU je CBA ilyokubaliwa na TPAWU itaendelea kutumika au ndo inakufaaa? mpaka TUICO wakae upya na kukubaliana tena na mwajiri?