Msaada wa kisheria jamani

Msaada wa kisheria jamani

ytara jr.

Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
61
Reaction score
22
Mimi ni mwalimu, nina miaka mitano kazini katika ngazi ya diploma.

Mwezi wa pili mwaka huu, kama (zilivvyo taratibu za halmashari nyingine) niliomba halmashaurini kwangu waniingize kwenye mpango wa kwenda kujiendeleza mwaka huu wa masomo 2015/16.

Kopi ya barua ninayo iliyosainiwa, ila sijaingizwa kwenye mpango, wenzangu hata wenye miaka miwili wameingiza kwenye huo mpango na wanaondoka masomoni.

Nimeenda hadi kwa mkurugenzi amesimamia hapo kuwa sipo kwenye mpango.

Nimejaribu kudodosa sababu nimegundua eti mkuu wangu wa shule ameongea na watu wa halmashaurini kwangu nisiondoke eti hana mwalimu mwingine wa sayansi.

Sasa niliomba mkopo bank kwaajili ya ada na mahitaji mengine, yani ki_ujumla nimejiandaa kwa 100%.

Ninachokiomba mnisaidie kisheria hii imekaaje, nikilazimisha nini kitatokea na nikisogeza mwakani wasiponiweka kwenye huo mpango tena?

Namba yangu ni 0757966585.

Msaada tafadhali.
 
Back
Top Bottom