Ipo hivi, jana asubh saa12 iliingia sms kwa namba ngeni, sms inasema hv "cm yangu ilichukuliwa jana usiku, usiitumie ujumbe, na hii niliyoitumia ni ya mama mdogo wake na jamaa usiitumie ujumbe" nami nikakaushaaa, maana ukiwa mwizi lazima ufate kanuni na masharti katika mawasiliano.
Ilipofika saa tatu na nusu za asubh, simu ya yule mwanamke ilitumika kunitumia ujumbe mfupi ukisema
"Kumbe huwa mnasoma mazngra eee...... Ndugu cha mwenzio ni kigumu meza mate ukalale""
Nikavunga siijui namba hyo maana nilitonywa mapema kuwa cm ilichukuliwa, nami nkajikakamua nikamuuliza kwa sms ikisema:-
"Namba ngeni, ujumbe mgeni, nani mwenzangu?"
Jamaa kupitia namba hyohyo ya mwanamke akajibu akisema:-
"Usijitoe ufaham nakujua unanijua"
Nami nikaona nisisalende ili niendelee kupoteza lengo as if amekosea no, nikamjibu ifuatavyo:-
"Kama hutaki kusema wewe ni nani kausha, maana namba ngeni, ujumbe mgeni na hutaki kusema ww n nan, huenda ukawa umekosea namba"
Alhamis, nilichart na huyo mwanamke kuna sms nilimtumia nikimwambia "Yaan ww na uelewa wote huo unayumbishwa na kauli za hao wambea?"
Jamaa akaquote sms yangu na kuijazilishia maeneno kuwa:-
"Wala si wambea, siku zote mbaya hakai akachunguza ubaya wake, wewe unavyo chukua wake za watu unadhan unatenda vyema?"
Nami nikamuuliza, "mke ama wake za watu wapi wanaochukuliwa na mimi?''
Akanyamaza nami nkapga kimya,
sasa mke kanyang'anywa cm, hatuwasiliani ama kuonana, sasa jamaa huwa yupo senta moja hv anabiashara yake, sasa najiuliza, kwakuwa ameshanitambua, niende nikamuombe samahan? Ama nipge kimyaa!?
Sasa kingne huwa anabiashara, leo nilipta maeneo fulan nikakuta kamchukua dogo wa nyumban amempa kkaz fulan kama kibarua, dogo huyu nilikuwa nmemuachia kaz nyumban, ikabidi nmfate pale kumuuliza kama kaz ya nyumban amemaliza, nae akasema bado nikamwambia fanya haraka ukaimalizie,,,,,,,, ila nilipofkapo tulikuwa wawili, jamaa aliitikia salam ya mwenzangu lakini yangu hakuitikia, na wakati huo hakutaka kutuface usoni.......... nikaona c tabu, sasa tulipotokapo, jamaa akamuuliza dogo, huyo fulan (akataja jina langu) n nan yako? Dogo nae akajibu n kaka angu......
Sasa MUUNGWANA, UNGEKUWA WEWE UNGEFANYAJE?............