Kifungu sikijui, ila sheria inatamka kuwa mtuhumiwa yeyote anatakiwa apandishwe kizimbani ndani ya masaa 48 tokea atiwe nguvuni. Akiishapandishwa kizimbani(kufikishwa mahakamani na kusomewa shitaka), mahakama itaamua kama aende mahabusu(magereza) au kama masharti ya dhamana kama yapo. Akienda magereza jukumu hilo linakuwa la serikali kupitia jeshi la magereza. Hivyo basi, polisi wakimuweka mtu rumande zaidi ya muda unaoruhusiwa kisheria walipaswa kumuhudumia wao ila kibongo bongo hakuna kitu kama hicho, utafia hapo kama huna ndugu
NB: Inategemea na aina ya kesi. Mfano kama ni kesi ya madai mlalamikaji ndiye anayetakiwa kumuhudumia mshtakiwa akiwa polisi au magereza. Hapa napo kibongo bongo hakuna kitu kama hicho. Tena ukijidai unajua sana kudai haki wakati upo chini ya polisi unawegeuziwa kesi ikawa ya utapeli hivyo ukakosa haki ya kumdai mlalamikaji kukuhudumia
Sent using
Jamii Forums mobile app
Katika mashauri ya jinai ni jukumu la jamuhuri kumhudumia mahabusu aliyeko ktk mikono ya vyombo vya dola iwe ni polisi ama magereza. Lakini ktk mashauri ya madai itakuwa ni jukumu la mdai kuhakikisha kwamba mdaiwa anahudumiwa ipasavyo iwapo mdaiwa itakuwa katiwa nguvuni polisi ama gerezani.
Naomba kuwasilisha!