Msaada wa kisheria: Je, jukumu la kumtunza/kumlisha mtu aliye Lumande ya Polisi ni nani?

Duniahadaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
336
Reaction score
677
Je, jukumu la kumtunza/kumlisha mtu aliye rumande ya Polisi ni nani?

Ni polisi, ndugu au walalamikaji?

Ukiweka sheria na kifungu husika itapendeza zaidi.

NB: Hapa namaanisha mtu aliye rumande miezi kadhaa na hajapelekwa mahakamani.
 
Kifungu sikijui, ila sheria inatamka kuwa mtuhumiwa yeyote anatakiwa apandishwe kizimbani ndani ya masaa 48 tokea atiwe nguvuni. Akiishapandishwa kizimbani(kufikishwa mahakamani na kusomewa shitaka), mahakama itaamua kama aende mahabusu(magereza) au kama masharti ya dhamana kama yapo. Akienda magereza jukumu hilo linakuwa la serikali kupitia jeshi la magereza. Hivyo basi, polisi wakimuweka mtu rumande zaidi ya muda unaoruhusiwa kisheria walipaswa kumuhudumia wao ila kibongo bongo hakuna kitu kama hicho, utafia hapo kama huna ndugu
NB: Inategemea na aina ya kesi. Mfano kama ni kesi ya madai mlalamikaji ndiye anayetakiwa kumuhudumia mshtakiwa akiwa polisi au magereza. Hapa napo kibongo bongo hakuna kitu kama hicho. Tena ukijidai unajua sana kudai haki wakati upo chini ya polisi unawezageuziwa kesi ikawa ya utapeli hivyo ukakosa haki ya kumdai mlalamikaji kukuhudumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…