Nina ujauzito wa mtu ambae baada ya kugundua nina ujauzito akaanza visa vya kunikwepa na kunikana.
Sasa naona anataka anitelekeze na kuniachia majukumu mwenyewe. Amesema nijifungue kisha tutaongea na kuna muda hataki kabisa kugusia hilo swala.Ujauzito ni wa miezi mitano.
Nilikua na ndoa ila tulitengana ndipo nikajikuta niko na huyu bwana,
Je nikijifungua haki za mwanangu ni zipi? Niko tayari kupima vinasaba ili ajihakikishie kua yeye ndie mzazi wa mtoto atakae zaliwa maana kuna wakati alianza kuleta maneno kua haniamini.
Kikubwa ninachohitaji ni matunzo kamilifu kwa mtoto.
Naomba msaada juu ya hili.