Msaada wa kisheria juu ya matunzo kwa mtoto asie wa ndoa

Pole sana aisee, kama huyo mtu anaroho ya kibinadamu atamtunza vizuri mtoto wake, ila kama akili zake fyatu sheria haina msaada sana, bado iko kikandamizi zaidi kwa wanawake,kiasi atakachopaswa kutoa ni kidogo sana kulinganisha na hali halisi, kiufupi sheria haijatambua bado thamani ya muda ule ambao utakua unautumia kulea mtoto huku aliyekupa mimba akiendelea na majukumu yake ya kiuchumi lakini sheria inasema matunzo ni asilimia 50 kwa 50, huwa nawachukia sana wanaume wanaokimbia majukumu yao ya malezi kwa watoto.
 
Kulea mtoto ni wajibu wa wazazi ndio maana hata wengi walikubali (hata kwa shingo upande) yale mashauri ya kwa Mkuu wa mkoa wa D'salaam.
 
Jiandae kulea huyo mtoto peke yako mkuu, maana hapo hana uhakika.

Kakuambia kuwa ukijifungua mtaongea ili ukizaa apate uhakika kama ni wake
 
Shukrani Baraza, ningefurahi karma mngejibu bila jazba wala hasira.Maana swali limeandikwa bila hasira. Maoni yenu woteeee ni muhimu na yanazingatiwa sana.
By the way mwenzenu ni mwanafunzi wa LAW SCHOOL ila nimeuliza hapa jukwaani kwa makusudi maalum. Wasalaam
 
So huna mimba ila ulikuwa unatuchora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…