Msaada wa Kisheria juu ya Ndoa na Mali.

everlenk

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
11,628
Reaction score
15,027
Habari za jioni wanasheria !!

Ndugu wanajukwaa nimekuja kwenu naamini hapa nitapata msaada,Nina ndugu yangu ambaye mume wake ametangulia mbele ya haki,Enzi za uhai wake marehemu alijaliwa kuwa na Mali kadhaa ambazo zote aliziandika majina ya ndugu zake,mama aliyeachwa ni mama wa nyumbani amebaki hana matunzo yoyote toka kwa familia,ameachiwa watoto watano,afanyeje angalau aweze kupata chochote kutoka kwenye Mali za mumewe ili aweze kuwatunza watoto wake, Marehemu hakuacha wosia wowote .

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 

Aliziandikaje kwa ndugu zake. Aliwauzia au alikuwa anazinunua kwa majina ya ndugu zake. Ufafanuzi ni muhimu hapo.
Kwa nini hakumpa mke wake , lzm kuna sababu ingawa zinaweza zidiwe na legal effect or value
 
Hii ngumu sana "Document speak for itself" na hata akiteuliwa msimamizi wa mirathi hawezi gawa kisichokua cha marehemu' kitendo cha marehemu kuwaandika ndug zake inamanisha anawapa uhalali kisheria wa umiliki wa mali zake. Kisheria itasumbua sana hii labda morality iaaply hapo na hao ndug wawe watu wa huruma. Mtazamo wangu[emoji57] [emoji57] [emoji57]
 
Aliziandikaje kwa ndugu zake. Aliwauzia au alikuwa anazinunua kwa majina ya ndugu zake. Ufafanuzi ni muhimu hapo.
Kwa nini hakumpa mke wake , lzm kuna sababu ingawa zinaweza zidiwe na legal effect or value
Mfano kwenye nyumba alikuwa anajenga nyumba kisha document zote anaziandika jina la ndugu yake,anaanzisha maduka mwisho wa siku anakuja kumilikisha ndugu yake,yeye ndo mmiliki lakini katika maandishi anaweka hivyo, huko nyuma waliwahi kupitia mgogoro wa kindoa ambao mwisho wa siku walifikia kuachana takribani miaka miwili hawakuwa wanaishi pamoja na ndo hicho kipindi Yule mume wake alibadilisha Mali zake nyingi na kuzifanya za ndugu zake akihofia kwamba ikifikia wakati wa taraka Yule mama asipate chochote lakini mwisho wa siku walikuja sameheana na maisha yakarudi kama mwanzo,lakini yule Bwana aliendelea kuziacha Mali zake zisomeke hivyo kasoro duka moja tu ndo lilikuwa na document zake na mwisho wa siku lile duka lilikufa na Mali zilizokuwepo mule zikahamishiwa sehemu nyingine(hapa alikuwa bado hai)
 
[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 

Kama alizinunua na kuandika kwa ndugu zake, si rahisi kuzipata. Labda kama kuna mali zilizokuwa zinajulikana za ndoa akazigawa hizo anaweza kuzidai akazipata maana aliziuza bila ridhaa ya mke wake. Vinginevyo ni ngumu sana kuzidai.
 
Imekula kwake Hugo mama. Aombe asali ili Rehema ya mungu iwapate waliomilikishwa kihalali. Lakini Hugo mzee alikuwa Mnyama sana. Unaoaje mwanamke anakuwa golikipa tu wakukaa nyumbani halafu humwandikishi chochote
 
Kwenye ndoa kuna mambo mengi sana na wanawake wa siku hizi wamekuwa tofauti sana na wale wa zamani wako radhi kukufanyia lolote mradi tu awe na uhakika wa kurithi mali.
Naamini huyo mwanaume hakuwa bwege ama taahira ninadhani alipokuwa akifanya hayo alikuwa na akili timamu na alikuwa anajua kuwa ana watoto ila siri ya yote marehemu atakuwa anajua.
Nitatoa mfano:
Kuna tukio lifafanalo na maamuzi kama haya wanaume tunajifunza, kuna jamaa alikuwa mfanyabiashara mzuri sana na alikuwa na mafanikio pale mitaa ya dumila. Lakini bahati mbaya hakuwahi pata mtoto kutoka kwa mkewe wa ndoa.! Isipokuwa kabla ya ndoa aliwahi kuwa na mtoto mmoja wa kiume. Hivyo akaamua kumchukua yule kijana ndio akawa akisaidia kuendesha biashara na wazazi wake,
Wakati kijana akiwa busy kwenye kuinua kiwango cha uchumi wa familia kumbe mama anapanga kumuua ili yeye ndo awe mrithi,
Siku kadhaa baadae akatega sumu kwenye chakula akitaraji dogo akirudi kula ale afe,! Lakini bahati mbaya aliye wahi kurudi nyumbani alikuwa baba mtu, na wakati mama analazimisha kuwa kile chakula cha mtoto baba mtu akang'ang'ania kula. Dogo anafika anasikia baba na mama wanazozana kuhusu chakula, dogo akamwambia acha baba ale mi nimekula chips bila kufikiri nasikia mzee akafakamia chakula haikuchukua mda. Mama anahaha huku na kule baba anatapatapa. Haikuchukua muda yule jamaa akafariki kabla hajafika hosptal.
Katika mazingira kama haya..wewe mwanaume unakuwa na ujasiri wa kufikiria kumrithisha mkeo kweli ?
 
Kama alizinunua na kuandika kwa ndugu zake, si rahisi kuzipata. Labda kama kuna mali zilizokuwa zinajulikana za ndoa akazigawa hizo anaweza kuzidai akazipata maana aliziuza bila ridhaa ya mke wake. Vinginevyo ni ngumu sana kuzidai.
Kuna Mali ambazo zilikuwa zinajulikana toka walivyoanza maisha ambazo hapo awali hata mama alizitambua ni zao lakini mwisho wa siku baada ya kifo cha mumewe kidocument zaonesha siyo za mumewe, kuna baadhi ya Mali mama alijua zimebadilishwa lakini alikuwa akihofia kumuuliza mumewe sababu asijeonekana ana tamaa ya mali,na kipindi chote cha migogoro yao yule baba alikuwa akimwambia hana chake pale.
 
Ni kweli kabisa watu wamebadilika sana sasahivi pande zote haziaminiki siyo wanawake siyo wanaume,lakini pia wapo watu ambao wamekuwa wakiishi tu kwa inferior complex akidhani kwamba akimilikisha mwanamke Mali atazichezea na kuwaachia vidume wengine wafaidi so anaona bora awape ndugu zake kuliko mkewe,na wengine dhana yao kwamba mke siyo ndugu yako saa yoyote atakugeuka sasa Anawaamini ndugu zake kwamba watatunza watoto wake kumbe mwisho wa siku ndugu nao utu hamna.
 

Km ni Muislam basi urithi utaenda kwa watoto wake n thelutu ya urithi atapa mke,marehemu km wazazi wake(baba n mama) yake wapo hai basi nao wanapata urithi
 

Akusanye ushahidi hata watu, wanandugu ambao walishuhudia akizihudumia hizo mali kama za familia anawezajenga argument na ushahidi huo kui convince mahakama.
 
Akusanye ushahidi hata watu, wanandugu ambao walishuhudia akizihudumia hizo mali kama za familia anawezajenga argument na ushahidi huo kui convince mahakama.
Na watu gani labda ambao anaweza kuwakusanya?,mfano kwa upande wa familia ya mumewe wote wako kinyume naye maana wao ndo walipewa Mali hizo so kiuhalisia hakuna ambaye yuko tayari kuusema ukweli.
 

Ndio maana nilimuuliza kwa nini mume alifanya hivyo. Ana sababu
 
Kama kuna chochote mume aliuza kwa jina lake bila sahihi ya mke, hicho dai atakipata
 
Inaonekana hakuwa na mbegu za kumzalisha mkewe ila ikawa siri ya wawili na kwamba wasizae ila mwanamke akaamua kucheza offside na kuzaa. Mwanaume kwa kuwa alikuwa na hela mwanamke akakaa kimya kusubiri mali kumbe mwanaume akaona bora wafaidi ndugu.
Najaribu kutegua kitendawili kama tulivyokuwa tukijibu maswali baada ya kusoma RIWAYA.
 
Na watu gani labda ambao anaweza kuwakusanya?,mfano kwa upande wa familia ya mumewe wote wako kinyume naye maana wao ndo walipewa Mali hizo so kiuhalisia hakuna ambaye yuko tayari kuusema ukweli.

Hata majirani wema ambao walishuhudia mkiishi kama mke na mume na kuzihudumia mali hizo kama za ndoa, ingawa inahitaji ujasiri wa majirani kujitokeza AU wasimamizi wa ndoa mahakama inaweza kuwaamini kama watu wenye uwezekano mkubwa wa kujua mambo ya ndani ya ndoa, itategemea uwexo wa kujenga hoja
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] tafsiri yako balaa!! Kuna watu tu asili Yao ni wabinafsi........ Asante kwa mchango wako.
 
Ujeuri Mbaya sana kama mali zina majina ya hao Ndugu huyo mama kwanini hataki kujielewa... ndio hivyo imekula kwake...

Kuna Dogo wa mbunge maarufu sana Musoma yeye ni toto la nje ya Ndoa ila one day alimkana babake na kukataa kusoma babake ni mwanasheria tokea enzi za mchonga akamuambia andika kwa maneno mimi sio baba yako toto linaandika na kusign... baba mtu akamfuta kwenye list ya watoto wake na toto lilivyo jinga ati likamvulia suruali babake akamuonesha makalio yake ati anamlaani babake... laana ikamrejea mtoto akawa choko hali mtaani na kwa mamake ikawa tete akawa anaomba msamaha kupitia kwa watu lakini dingi limekaza tu likikumbuka ila baadae akamsamehe ila ndio sio tena mwane na akimsaidia ni pesa za kula siku mbili tatu sasa toto limekuwa jitu zima maisha ni kupiga mizinga tu.. nachukia sana watu wajeuri kiasi hiko.. maana inafikia hata mtu kusamehe kirohoni inakuwa ngumu naiabaki juu juu... Mungu Atusamehe sometime hawa hatujielewi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…