Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] tafsiri yako balaa!! Kuna watu tu asili Yao ni wabinafsi........ Asante kwa mchango wako.
Asante sanaHata majirani wema ambao walishuhudia mkiishi kama mke na mume na kuzihudumia mali hizo kama za ndoa, ingawa inahitaji ujasiri wa majirani kujitokeza AU wasimamizi wa ndoa mahakama inaweza kuwaamini kama watu wenye uwezekano mkubwa wa kujua mambo ya ndani ya ndoa, itategemea uwexo wa kujenga hoja
Siyo ujeuri ndugu yangu ni namna ambavyo anajaribu kuwasaidia watoto wake ingelikuwa siyo watoto Hata asingefuatilia chochote mbaya zaidi ndugu za mumewe ndo hivyo hawataki kuwasaidia watoto.Ujeuri Mbaya sana kama mali zina majina ya hao Ndugu huyo mama kwanini hataki kujielewa... ndio hivyo imekula kwake...
Kuna Dogo wa mbunge maarufu sana Musoma yeye ni toto la nje ya Ndoa ila one day alimkana babake na kukataa kusoma babake ni mwanasheria tokea enzi za mchonga akamuambia andika kwa maneno mimi sio baba yako toto linaandika na kusign... baba mtu akamfuta kwenye list ya watoto wake na toto lilivyo jinga ati likamvulia suruali babake akamuonesha makalio yake ati anamlaani babake... laana ikamrejea mtoto akawa choko hali mtaani na kwa mamake ikawa tete akawa anaomba msamaha kupitia kwa watu lakini dingi limekaza tu likikumbuka ila baadae akamsamehe ila ndio sio tena mwane na akimsaidia ni pesa za kula siku mbili tatu sasa toto limekuwa jitu zima maisha ni kupiga mizinga tu.. nachukia sana watu wajeuri kiasi hiko.. maana inafikia hata mtu kusamehe kirohoni inakuwa ngumu naiabaki juu juu... Mungu Atusamehe sometime hawa hatujielewi...
Ukiona marehemu hakuona umuhimu kuhusu watoto bila shaka alikuwa na walakini kuhusu uhalali wa watoto hao kuwa wake.Siyo ujeuri ndugu yangu ni namna ambavyo anajaribu kuwasaidia watoto wake ingelikuwa siyo watoto Hata asingefuatilia chochote mbaya zaidi ndugu za mumewe ndo hivyo hawataki kuwasaidia watoto.
Ni kweli kabisa haya mambo yapo,ila Uzuri kwa upande wao aisee hata macho yadanganyi watoto wote ni copy&paste ya baba,Yule shemeji yetu alikuwa mkatili tu alikuwa anaona mwanamke akimiliki Mali atamzidi akili sasa matokeo yake ndo hivyo aliowaamini wamemuangusha.Ukiona marehemu hakuona umuhimu kuhusu watoto bila shaka alikuwa na walakini kuhusu uhalali wa watoto hao kuwa wake.
Ajuae ukweli kuhusu mimba na watoto ni mwanamke.!
Kuna wanaume wabinafsi sanaKuna Mali ambazo zilikuwa zinajulikana toka walivyoanza maisha ambazo hapo awali hata mama alizitambua ni zao lakini mwisho wa siku baada ya kifo cha mumewe kidocument zaonesha siyo za mumewe, kuna baadhi ya Mali mama alijua zimebadilishwa lakini alikuwa akihofia kumuuliza mumewe sababu asijeonekana ana tamaa ya mali,na kipindi chote cha migogoro yao yule baba alikuwa akimwambia hana chake pale.
Usihukumu maana huwezi jua yamkini huyo mama awali alitenda unyama sana sasa jamaa kajihami,Imekula kwake Hugo mama. Aombe asali ili Rehema ya mungu iwapate waliomilikishwa kihalali. Lakini Hugo mzee alikuwa Mnyama sana. Unaoaje mwanamke anakuwa golikipa tu wakukaa nyumbani halafu humwandikishi chochote
InaumizaKwenye ndoa kuna mambo mengi sana na wanawake wa siku hizi wamekuwa tofauti sana na wale wa zamani wako radhi kukufanyia lolote mradi tu awe na uhakika wa kurithi mali.
Naamini huyo mwanaume hakuwa bwege ama taahira ninadhani alipokuwa akifanya hayo alikuwa na akili timamu na alikuwa anajua kuwa ana watoto ila siri ya yote marehemu atakuwa anajua.
Nitatoa mfano:
Kuna tukio lifafanalo na maamuzi kama haya wanaume tunajifunza, kuna jamaa alikuwa mfanyabiashara mzuri sana na alikuwa na mafanikio pale mitaa ya dumila. Lakini bahati mbaya hakuwahi pata mtoto kutoka kwa mkewe wa ndoa.! Isipokuwa kabla ya ndoa aliwahi kuwa na mtoto mmoja wa kiume. Hivyo akaamua kumchukua yule kijana ndio akawa akisaidia kuendesha biashara na wazazi wake,
Wakati kijana akiwa busy kwenye kuinua kiwango cha uchumi wa familia kumbe mama anapanga kumuua ili yeye ndo awe mrithi,
Siku kadhaa baadae akatega sumu kwenye chakula akitaraji dogo akirudi kula ale afe,! Lakini bahati mbaya aliye wahi kurudi nyumbani alikuwa baba mtu, na wakati mama analazimisha kuwa kile chakula cha mtoto baba mtu akang'ang'ania kula. Dogo anafika anasikia baba na mama wanazozana kuhusu chakula, dogo akamwambia acha baba ale mi nimekula chips bila kufikiri nasikia mzee akafakamia chakula haikuchukua mda. Mama anahaha huku na kule baba anatapatapa. Haikuchukua muda yule jamaa akafariki kabla hajafika hosptal.
Katika mazingira kama haya..wewe mwanaume unakuwa na ujasiri wa kufikiria kumrithisha mkeo kweli ?