Msaada wa kisheria juu ya utoroshaji wa mwanafunzi

Msaada wa kisheria juu ya utoroshaji wa mwanafunzi

Okinyit

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
6
Reaction score
2
Habari wana Jamii,

Kwa heshima na taadhima naombeni msaada wa mawazo (Kisheria) katika hili.

Mwishoni mwa mwezi wa tatu mdogo wangu anayesoma kidato cha nne alipotea nyumbani majira ya saa 2 usiku na hakuonekana hadi baada ya siku 3.

Kabla hajaonekana wakati tupo kwenye pilika za kumtafuta, tulifanikiwa kukuta sms za mawasiliano kati yake na mwanaume ambaye tunamfahamu.

Tulimkamata na kumfikisha Polisi na alikiri kumtorosha huyo binti na ushahidi wa sms kwenye simu yake na ya mama yetu ambayo mdogo wetu alitumia kuwasiliana naye.

Mashahidi wapo 3 waliyomwona. Sasa tatizo ni kwamba inaonekana Mkuu wa Kituo cha Polisi amepewa hela analazimisha tulimalize kishkaji na jamaa ila nimegoma baada ya kukataa amekasirika sana na kutishia kwamba kwanza kosa la kumtorosha mwanafunzi siyo lazima mtu afungwe maisha.

Anadai nakataa hela nawaachia wengine (akimaanisha hakimu), na ameshamwandaa Hakimu kwa kushirikiana na ndugu wa mtuhumiwa ambaye naye ni Polisi Mikumi. Naomba kujua yafuatayo:

1. Je, kosa la kumtorosha mwanafunzi ni jinai au si jinai?
2. Je, mahakama ya mwanzo inayo uwezo wa kisheria kulisikiliza?
3. Je, nina haki ya kuchagua mahakama pa kupeleka kesi kwa sababu hii iko mita 150 toka kituo cha Polisi na kuna kila dalili Hakimu washamwandaa.

Je, naweza kumkataa Hakimu?

Nawasilisha.
 
binti mwenyewe ana umri gani kwanza
1. Kosa ni jinai
2. Mahakama ya mwanzo haina uwezo, bali mahakama ya wilaya
3. Kwakuwa kosa ni jinai na lina uwezo wa kusikilizwa na mahakama ya wilaya hivyo wakili wa serikali ndiye atakayeandaa charge baada ya kuwa wamepelekewa jalada kutoka polisi la malalamiko yako, na uyo wakili wa serikali ndiye atakayesimamia kesi yako. Wewe unaweza kuitwa kama shahidi tu.
huyo hakimu ambaye unataka kumkataa ni wa mahakama ipi? Kwa kuwa kesi zote mahakamani kwa kila hakimu zinakuwa assigned kwao na hakimu mfawidhi wa mahakama husika.
 
Back
Top Bottom