Mpambalachuma
JF-Expert Member
- Apr 4, 2015
- 362
- 44
wanakuja wataalamu.
Subiri hapo hapo
njoo ofisini,hapa hakuna ushaur wa bure
Wakuu, mim mzee wangu alitukanwa na kudhalilishwa, baada ya hapo akashitakiwa mahakama ya mwanzo lkn akashinda kesi hiyo, cha ajabu mlalamikaji anadai hakuridhishwa na mahakama hivyo kakata Rufaa, so naomba mnisaidie hapo kesi itakuwaje!?
Ujatuambia mzee alishitakiwa kwa kosa gan mkuu tuanzie hapo kwanza.
Baada ya mzee kupita ktk uchaguz wa Serikal Za mitaa Kwa tiket ya Chadema mkoani Tabora, wale walioshindwa ktk uchaguz huo wakamtolea maneno ya kashfa "we mwenyekiti umeokotwa tu" ndio mzee akawaambia "mnagongwa na mimi" then akaondoka, baada ya hapo akashitakiwa ktk mahakama ya mwanzo ambapo mahakama ilimwachia huru Kwa kumuona Hana hatia ya kutenda Kosa Hilo huku mahakama ikitoa ufafanuzi juu ya neno kugonga, ambapo wakasema ni kupiga kitu, Sasa baada ya hukumu hiyo mlalamikaji akaamua kukata Rufaa, ambapo mzee ametakiwa kufika mahakama tar 28 mwez huu.
Sikia mkuuu hilo neno alilowaambia mzee wako hao watu wengine kwamba WANAGONGWA halina maana yoyote kwenye macho ya sheria kama tunavyomaanisha huku mtaani mahakama inatafisiri hilo neno kwamba kama kugusa kitu fulani neno UNAGONGWA halitoshelezi kumuhukumu mtu kwa kutoa lugha za matusi. Jambo la msingi ukumbuke rufaa ni haki ya msingi ya kila mtu waache wa appeal na nawasihi nendeni mahakamani siku ya kusikiliza appeal hyo (rufaa) natumaini itakuwa ni mahakama ya wilaya kama hakuna neno lolote ambalo alitoa mzeee ambalo linaashiria lugha ya matusi direct usiwe na wasiwasi kwa sababu kwenye Appeal hakuna kesi mpya ambayo itafunguliwa zaidi ya fact zile zile zilizokuwepo kwenye kesi ya kwanza mahakama ya mwanzo kupitiwa upya.
Krbu tena.
nimekimbia kusoma hayo maneno usikute mpambala CHUMA anamaanisha hapa JF
Hayo maneno 'mnagongwa na mimi' hayana maana ya matusi na sizani kama kuna sheria inayo weza ya fafanua yakawa na maana ya tusi.
Kwaupeo wangu tu huu wa kawaida usio wa kisheria na amini mzee wako atashinda kesi tena.
Hapo kesi itakuwa kama ilivyo kuwa mahakama ya mwanzo. mzee wako ataendelea kushitakiwa kwa kosa hilo hilo lilitolewa hukumu mahakama ya mwanzo.
Wanàsheria watàkusàidia zàidi. Nime muona Mr.Penal Code, atakupa majibu.
Hofu yako nini hiyo ni rufaa tu mlalamikaji anahisi huko mbele atapata haki zaidi hakuna jipya,ila manguli wa sheria watakupa ushauri.
Usitatizwe na kuhonga. Maneno yalio tamkwa na kufunguliwa shitaka hayana maana ya matusi. Mshitakiwa hana kesi ya kujibu hapo.
Wazoefu wakushinda mahakamani baada ya kufunguliwa kesi kama hizi, wakishinda huwa wanafungua kesi ya madai.
Mtafute Mch. Mtikila akupe msaada.