Msaada wa kisheria Kuhusu ardhi

The Transporter

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
3,580
Reaction score
7,203
Habari za jumapili wadau,
niende kwenye hoja moja kwa moja
nilibahatika kununua kaeneo sehemu aliyeniuzi sasa ni marehemu Mungu kampenda zaidi ila yeye halikuwa eneo lake alikabithiwa tu kuuza na mwenye eneo kwa makubaliano ya kupeleka salio kwa muhusika inasemeka marehemu hakuwa anapeleka salio kwa muhusika japo wakati anatuuzia muhusika alikuwa anakuja na hajawahi kusema chochote zaid ya miaka mitano maana hakai mbali na ana mwanae pia hakai mbali na eneo lililouzwa ila baada ya aliyeuza kufa anataka kuja kudai eneo lake na eneo limeshakuwa mji kisheria imekaaje hii?
 
1.Hati/fomu za mauzo na manunuzi ya kiwanja zilifuata utaratibu wa kisheria?

2.Serikali ya mtaa & mashahidi wa pande zote walihusika na kumbukumbu zipo?

Kama majibu ni ndio....
Na unaona hakuna dalili za maridhiano na thamani ya ardhi haizidi M3 Nenda baraza la ardhi la kijiji/mtaa...kama inazidi M3-40 anzia Baraza la ardhi la kata!

Kama inazidi 40M anzia Baraza la ardhi na nyumba la wilaya,usiporidhika nenda mahakama kuu kitengo cha ardhi usiporidhika Nenda mahakama ya rufaa ya Tanzania.kote huko ukifel itabidi wapatikane wataalam washeria za kimataifa wakushauri cha kufanya Nje na Sheria za Tz.

Rejea:
1.Sera ya Taifa ya ardhi ya 1995
2.Sheria ya ardhi Na.4 ya mwaka 1999
3.Sheria ya ardhi ya vijiji Na.5 ya mwaka 1999
4.Sheria ya mahakama za kushughulikia migogoro ya ardhi Na.2 ya mwaka 2002 n.k
 
wanakujaaa....

[HASHTAG]#Atubu[/HASHTAG]
 
asante mkuu taratibu zote zilifatwa ikiwemo mjumbe mpk serikali ya mtaa na document zipo na mashahidi wapo.
 
Tafuta ushaidi wa kudhihirisha kwamba, alijua uuzwaji huo na aliridhia, then anza naye kwenye ngazi ya chini kabisa ya utatuzi wa migogoro.... Mtaa au kijiji.
 
Najua ni ngumu kumeza ila kuna miiko ulikiuka kulingana na maelezo yako mwenyewe hapo juu.

Katika miiko ile "Buyer Beware" inashauriwa kuwa usikubali anayekuuzia ardhi asiwe ndiye mmiliki halisi wa ardhi hiyo, na kama hati ipo basi hakikisha anayekuuzia ndiye aliyeandikwa hapo, kamwe usikubali hadithi za kiwanja ni cha Baba yangu, Mama yangu, mdogo wangu n.k.

Jaribu ushauri uliopewa hapo juu, ila kama huyo jamaa anafanya makusudi kwa kutumia udhaifu huo uliojitokeza basi anaweza kukusumbua kwa kweli, coz inaonyesha hana nia nzuri.
 
asante sana mkuu ni ngumu kweli kumeza duh
 
.
Mkuu, Mwenye mali ni mwenye mali tu. Eneo "ulilouziwa" linaweza kuwa lako kihalali endapo tu ulilipata/ulilinunua kutoka kwa mwenye mali. Huyo "uliyeandikishana" nae kama alikuwa na uwezo wa kuhamisha umiliki "pass title" kutoka kwa mwenye mali hadi kwako basi una haki na eneo hilo. vinginevyo hata ukihusisha mashahidi na serikali ya kijiji umiliki wako utakuwa na dosari kubwa kisheria.

Cha msingi hapa ni je, mmiliki halali alishirikishwa kikamilifu katika misingi ya sheria katika "mauziano" yenu? Ama la, basi je, uliyefanya nae mkataba alikuwa na mamlaka halali (hasa kisheria) kukuuzia kipande hicho cha ardhi?

Kataka sheria mtu hawezi kuuza kitu ambacho hana/hamiliki. Mwenye eneo hili anayo haki na vigezo vya kudai eneo lake, maana kwa maelezo yako inaonesha hakuliuza/hakukuuzia eneo.
 
Safi sanaa, ur so smart bro.

Akikujibu hapa basi tatizo lake litakua limeisha.
 
Yaani hapa umemaliza kabisa. plus that principle of "Buyer beware"
 
Hapa kuna tatizo limetokea, Mleta Uzi mwenyewe ameliweka tu bayana. Kwamba amenunua eneo toka kwa wakala wa mmiliki. Wakala Amefariki, mwenye mali analidai eneo lake. Mwenye uelewa wa hii fani amsaidie. Sio akae upande wa pili, hajakuomba msaada huo.

Mimi nimesema, kwamba lazima atafute ushaidi wa kuthibitisha kwamba alikuwa anajua biashara ilivyokuwa inaendeshwa juu ya eneo lake,,hilo tu.

Nazijua hizi changamoto, tena inawezekana aliyeuziwa ameshaishi hapo kwa miaka kadhaa hapo, ameshajenga nknk.
 
Marehemu alikuwa anasimama kama nani kwenye mkataba wa mauziano?
Jina na sahihi za mwenye mali halali zinatambulika kwenye mkataba wa mauziano?
Kama mwenye mali halali hakushiriki kabisa mchakato mzima wa mauziano ili kuwa ni lazima ampe muuzaji nguvu ya kisheria ya kuuza kwa niaba yake na ufanyike kwa mwanasheria kinyume cha hapo mkataba wa mauziano ni batili na ana haki kisheria kuwaondoa katika eneo lake. POWER OF ATTORNEY IPO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…