zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Jamani mtaani kwangu hakuna mjumbe wa Nyumba kumi aliye "official" lakini mara nyingi huwa kesi ndogo ndogo naletewa mimi kuzipatia ufumbuzi kutokana na umri wangu.
Kuna hii nimeletewa jana na nimeshindwa kuamua hapo kwa hapo na nimeomba nipewe muda kuipatia ufumbuzi, naomba msaada wa kisheria au kisharia kwenye hili:
Kuna mtu ana mwembe uwani kwake, ule mwembe uko karibu na ukuta wa uwa wa nyumbani kwake lakini kwa juu matawi yametokeza mpaka upande wa pili wa uwa ambako ni kwa jirani yake. Jirani anachuma maembe yanayoning'inia upande wake na anasema hiyo ni halali yake na mwenye mwembe anadai alipwe, jirani nae anasema basi kuanzia leo kama unataka nikulipe, na wewe uje kufagia majani na taka zingine za mwembe zinazodondokea uwani kwangu. Wakaamuwa waje niwatatulie hili kasheshe, nikawaomba wanipe siku tatu, sina ufumbuzi wa haraka.
Jumatano Jioni watakuja kwangu kupata ufumbuzi, naomba mwenye kuijuwa hukumu ya hili iwe kisheria au kisharia anisaidie.