msaada wa kisheria kuhusu employment contracts

msaada wa kisheria kuhusu employment contracts

baina

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
219
Reaction score
59
Samahani wanasheria naomba kufahamishwa kuhusu tatizo hili,

Kuna mwajiri (jina kapuni) anataka kubadilisha/kufuta mikataba ya wafanyakazi wenye ajira ya kudumu (a contract for an unspecified period of time) na eti awaingize katika mikataba ya muda maalum.
Hapa nashindwa kuelewa kama sheria ya kazi inaruhusu au hapana, na kama hairuhusu je msingi wa kulipa utakuwaje, na anaweza kuwa anavunja sheria kama atafanya hivo?

Msaada wa haraka.
 
Hapo kuna mambo mawili. Huyo mwajiri wako anataka kuvunja 'the existing contract' au anataka kufanya 'addendum' kwenye hiyo existing contract? Akivunja mkataba, hilo ni kosa kisheria as per Cap 345[r.e 2002] s.73 (1) na utapata mapesa ya kutosha tu ingawa hiyo itakua determined by the terms of ur contract. Na ikiwa anataka kufanya marekebisho ya aina yoyote ktk mkataba wako (addendum), kisheria hiyo addendum ndio utakua mkataba wako mpya, na ni lazima kwenye mkataba kuwe na free consent of the parties, (yaani wewe na mwajiri wako), so sheria inasema mkataba wowote ambao mshiriki amelazimishwa kuu-sign ni batili. Free consent inaelezewa vizur ktk Cap 345, s.14. Na vile ishu ya kusaini mkataba kwa matakwa yako ipo ktk section 10 ya cap 345. Natumain umeelewa.
 
hapo kuna mambo mawili. Huyo mwajiri wako anataka kuvunja 'the existing contract' au anataka kufanya 'addendum' kwenye hiyo existing contract? Akivunja mkataba, hilo ni kosa kisheria as per cap 345[r.e 2002] s.73 (1) na utapata mapesa ya kutosha tu ingawa hiyo itakua determined by the terms of ur contract. na ikiwa anataka kufanya marekebisho ya aina yoyote ktk mkataba wako (addendum), kisheria hiyo addendum ndio utakua mkataba wako mpya, na ni lazima kwenye mkataba kuwe na free consent of the parties, (yaani wewe na mwajiri wako), so sheria inasema mkataba wowote ambao mshiriki amelazimishwa kuu-sign ni batili. Free consent inaelezewa vizur ktk cap 345, s.14. Na vile ishu ya kusaini mkataba kwa matakwa yako ipo ktk section 10 ya cap 345. natumain umeelewa.

mkuu nakushukuru sana kwa msaada wako, ila naomba unisaidie kitu kimoja kwani mie si mwanasheria japo kimombo kinapanda, vipi waweza kuniandikia kwa marefu maana ya hapo kwenye red na je hiyo document naweza kuipata?. Zaidi ni kwamba huyu mwajiri anataka kufuta ajira za kudumu za wafanyakazi wake ambao ni sisi na eti kutuingiza ktk mikataba ya muda maalum, kwa maana nyingine ni kama vile anafuta mikataba yetu inayotuambia kuwa sisi ni wa mikataba ya kudumu.
 
Back
Top Bottom