Msaada wa kisheria kuhusu kesi hii

Msaada wa kisheria kuhusu kesi hii

texaz mc

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2016
Posts
371
Reaction score
205
Habari zenu wadau wote wa JF.
Kuna mtoto alifiwa na mama yake mzazi mwezi wa kwanza mwaka huu, sasa baada ya msiba kuisha mtoto huyo hadi leo hajawahi kushirikiswa kuhusu ugawaji wa mali ya mama yake. Msimamizi wa mirathi ambaye ni mjomba wake anataka kuuza nyumba ya mama wa huyo mtoto na wamekana kuwa MAREHEMU HAKUACHA MTOTO( YAANI HAKUWA NA MTOTO ).Ana umri wa miaka 17 sasa na anatarajia kuanza masomo ya advance mwaka huu, Usaidizi anaotaka ni kupiga stop uuzwaji wa hiyo nyumba kwana mpaka amalize advance then aje aendelee na hiyo kesi, je ni utaratibu gani afuate na aende wapi ili akamilishe mpango huo??? Na pia marehemu aliacha mali nyingine kama biashara lakini biashara hiyo bado inaendeshwa toka mwezi wa pili bila mtoto huyu kuhusishwa. MSAADA WENU UNAHITAJIKA PLZ
 
Duh Dunia inaviumbe katili aseh
 
Si aende polisi asema anadhulumiwa? au atafute wakili ampe dili tu.
 
albadir tu, hapo unaanza na hao ndugu, dalali, atakayeitamani nyumba,mnunuzi, atakayeishi humo, mifugo watakayofuga hata mpita njia atayeenda kuukojolea ukuta wote unawatia tezi dume
 
1.Kuwa msimamizi wa marithi haimaanishi wewe ni mmiliki au mnufaika wa mirathi

2.Weka hapa hukumu iliyompa mamlaka ya kusimamia mirathi tuangalie na mgao wa mirathi kama huyu mtoto amejumuishwa

3.Je! hata wanandugu hawamtambui huyo kijana? maana kabla ya kesi ya mirathi kusikilizwa lazima mahakama ifuate muhtasari wa kikao cha wana ukoo

4. Inamaana hata kikao kiligubikwa na ubaguzi bado dogo alikuwa na uwezo wa kuweka pingamizi mahakamani kuwa kikao cha wanandugu hakikuwa cha haki
 
1.Kuwa msimamizi wa marithi haimaanishi wewe ni mmiliki au mnufaika wa mirathimirathi
Kabla ya kifo chake huyo mama

2.Weka hapa hukumu iliyompa mamlaka ya kusimamia mirathi tuangalie na mgao wa mirathi kama huyu mtoto amejumuishwa

3.Je! hata wanandugu hawamtambui huyo kijana? maana kabla ya kesi ya mirathi kusikilizwa lazima mahakama ifuate muhtasari wa kikao cha wana ukoo

4. Inamaana hata kikao kiligubikwa na ubaguzi bado dogo alikuwa na uwezo wa kuweka pingamizi mahakamani kuwa kikao cha wanandugu hakikuwa cha haki
Yaani hata kwenye kikao hakuitwa, pia kkabla ya kifo wanandugu walikua wanamjua huyo mtoto, pia hata huyo mtoto ana cheti cha kuzaliwa chenye jina la huyo mama, pia wakati alipokuwa hai kwenye hati ya nyumba kulikuwa na pichA ya huyo mtoto na saini yake lkn siku moja baada ya kufariki kwa huyo mama ile hati iliibiwa( nadhani aliichukuwa huyo anaesimamia )
 
Inaweza akafanana na wale wanaojitokeza Dar. Lakini inategemea na sehemu pamoja na mila ,desturi pamoja na level ya uelewa ya kijana na jamii inayomzunguka. Namshauri mtoa mada kwa kuwa anamfahamu huyo kijana, na ana uwezo mpaka wa kuleta mada huku na kuchagua jukwaa basi amuongoze
 
Back
Top Bottom