Msaada wa kisheria kuhusu kuachishwa kazi

Mchina anashughulika na Uingizaji na utoaji mizigo kupitia bandari ya Dsm
 
HAPANA. Probation na terms zake zinapaswa kuwa kwenye MKATABA RASMI wa kazi.

Na kuna muda maalumu wa probation na masharti yake!

Ndio maana nikasema hapa panahitaji maelezo ya kina!...
Nimekuelewa vizuri, kilichonipanikisha n ile kuitosa kazi ingine ya mkoani sababu ya kwamba makazi yangu ya kudumu yapo mjini, sasa najaribu kurudi kwenye plan B (mkoani), naambiwa nafasi imeshajazwa na mtu mwingine, apo ndo nimeanza kuziona rangi za nyota, na kuona kama huyu amekua kama mchawi kwangu.
 
Je ni sahihi kuanza kufanya kazi pasipo mkataba ?
waelevu wa maswala ya kisheria watatusaidia, japo ninavoelewa mm sio sahihi, lkn je ni nani anawajibika kwa kutokuwepo kwa mkataba, ni mwajili au muajiliwa.
Naamini kuna wabobezi wengi sana wa maswala ya kisheria, ngoja tuone.
 
Wew una matatizo mwenye kazi kasema hufai unaanza kutafuta haki na mlikubaliana mi nadhan boss huyo aliona mbali badae ungemletea matatizo wew
 
kwahiyo ni sahihi kuanza kufanya kazi pasipo ni mkataba?
Aliyepaswa kudai mkataba ni nani? Why uone umuhimu wa mkataba baada ya kuachishwa kazi? Katika hizo wiki 2 kwa nini hukuona umuhimu wa mkataba?
 
Tatizo lipo kwako hukufanya maamuzi ya busara kwa kuangalia subject than objective. Ulipaswa kuangalia fursa zote mbili kwa ulinganifu wa mfano na utofauti then come up with sound conclusion.
 
Nilitegemea nitaambulia vifungu vya kisheria lkn naona kikubwa ninachokipata ni tathmini ya watu juu yangu binafsi, japo kuna wachache wameonesha kunielewa.

Imebidi nifanye jugudi za ziada na kuweza kupata kifungu cha sheria ambacho kimeniridhisha nadhani, sidhani kama kuna kingine zaidi ya icho nilichokiatach,

Jamii forum n jukwaa kubwa tuendelee kuliheshimu.

Ata mtu akikuuliza hivi nikifanya mapenzi na mtu ambae hana akili vizuri (kichaa), kisheria inakuaje ......... nadhani walio wengi watajielekeza kwenye 'kwnn ufanye mapenzi na kichaa' au 'wewe nae ni kichaa'

Lkn mm kwangu nionavyo sahihi n kupewa kwanza msaada wa kisheria aliouhitaji kisha kama kuna mambo yako binafsi nawe unayaweka ....... all the way this is our Tz.
 

Attachments

  • IMG_20200704_164842.jpg
    34.4 KB · Views: 4
Kama alikulipa kulingana na makubaliano, hujadhulumiwa.

Hapo yeye anaweza kusema kwa hizo wiki mbili, hujakidhi vigezo vya kupewa mkataba.

Yuko sahihi.
...na VIP kama alikatisha mkataba ndani ya week moja..I,e before probabiliin period kuisha.
Je,-kisheria imekaaje hiyo
 
...na VIP kama alikatisha mkataba ndani ya week moja..I,e before probabiliin period kuisha.
Je,-kisheria imekaaje hiyo

Hakukuwa na mkataba hapo, haja sign chochote. Ilikuwa makubaliano ya mdomo ambayo kisheria hayafungi.
 
..let's alipewa barua ya probation ya 3 months,.baada ya week 2 akapewa barua ya kuachishwa kazi kuwa hawataendelea naye...na hawajamuambia sababu hasa ni nini ?
...sheria ikoje hapo ?!
Hakukuwa na mkataba hapo, haja sign chochote. Ilikuwa makubaliano ya mdomo ambayo kisheria hayafungi.
 
Naomba kutoa Mchango wangu kama ifuatavyo

Kanuni za ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2007 na sheria za ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 zipo wazi kueleza wafanyakakazi waliopo chini ya muda wa majaribio na utaratibi wa kuwaachisha kazi

1. Mfanyakazi hata akianza kazi leo unatakiwa umpe mkataba ila sasa ndani ya huo mkataba utatakiwa kuonesha ni muda gani wa majaribio KANUNI YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2007 kifungu cha 10 inasema muda wa majaribio usipungue miezi sita na usizidi mwaka mmoja

sasa huu muda wa majaribio unampima kitu gani mfano umeajiriwa kama Sales Agent au representative utapimwa vitu vifauatavyo Sales target, Customer retention na reporting ila ukishindwa kuyafikia hayo muajiri wako lazima akuite akupe muda apate maelezo yako lazima aseme unakosea wapi nini unatakiwa kufanya ili uwe vizuri hayo yote yawe kwa mtindo wa maandishi

Pale itakapoonekana sasa hauwezekaniki ndipo utaambiwa umeshindwa muda wa majaribio tena kwa Maandishi sio kwa mdomo

kama hayo yote hayakufanyika maana yake walikikuka sheria

Hivyo unahaki ya kuwafungulia Kesi ila sasa changamoto hukuwa na kitu chochote cha kukutambulisha kama kielezo cha kuwa wewe ni mfanyakazi hapo ndipo changamoto itakopoanzia sasa ila kama ulipewa barua yoyote ile siku unaambiwa umeshindwa majaribio basi unaweza kuitumia kuanza kudai haki yako
 
Sasa mlikubaliana atakulipa hio probation period na amefanya hivo sasa hapo unadai nini tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…