Unaweza au usiweze kuzipata hizo pesa. Hili litategemea kama kulikuwa na mkataba kati yenu. Mkataba sio lazima uwe kwa maandishi. Ila ukiwa wa maandishi ni rahisi kudhibitisha. Pia inategemea kama ulimpatia hizo pesa kama zawadi au mkopo. Tatizo linakuja kwenye ushahidi. Hakuna maandishi (promissory note) kudhibitisha kuwa ulimkopesha na aka-promise kukurudishia hizo pesa baada ya muda fulani. Ulimpaje hizo pesa? Kwa hundi or bank transfer? If so, unaweza kutumia hizo kama ushahidi. Lakini kama ulimpa cash itakuwa ngumu unless kama kuna watu walioshuhhudia ukimkabidhi hizo pesa kama mkopo. Kati ya hizo milioni 5, hajawahi kukurudishia hata kidogo? Kama amekurudishia kidogo unaweza kutumia hiyo kama ushahidi kuwa unamdai ndio maana amekurudishia kidogo. Still bado ni ngumu na itategemea alikurudishia kwa njia gani.
Katika kukopeshana huko mlishawahi kuwasiliana kwa text messages or email? Kama kuna correspondences kama hizo unaweza kuzitumia kama ushahidi wa mazingira kujaribu kuonyesha kuwa ulimkopesha. Pia hizo pesa alienda kuzifanyia nini? Kwa mfano kama alizitumia kupata bail, then unaweza tumia hiyo bail kama ushahidi. Still hii bado ni ngumu. Kama huna ushahidi wowote kilichobaki labda yeye mwenyewe akubali kuwa unamdai. Otherwise, itakuwa vigumu sana kumshtaki na kushinda kesi. Anaweza akakataa au akasema tuu kuwa ulimpatia hizo pesa kama zawadi (gift). Hata kama una ushahidi wa kutosha, pia angalia kama huyo jamaa kama ana uwezo wa kulipa ukimpeleka mahakamani. Usije ukakuta unaingia gharama za bure na kupoteza muda wako.
Lakini nafikiri hapa utakuwa umepata fundisho ili usirudie kosa kama hilo. Sina maana kuwa usimkopeshe mtu tena kwa sababu iko siku na wewe utahitaji kukopa. Huwezi jua. Cha kujifunza hapa ni kwamba, next time ukikopesha jaribu kutengeneza ushahidi in case akikataa kulipa. Badala ya kumlipa cash tumia njia nyingine kama hundi au bank transfer kutoka kwenye account yako kwenda yake. Tengeneza mazingira ili mtumie mawasiliano ya kimaandishi zaidi wakati anaomba mkopo. Kuandikiana mikataba inategmea na mahusiono yenu na kiasi cha mkopo. Kama mkopaji anasisitiza umkopeshe kwa cash badala ya hundi or bank transfer, au anakataa kutumia aina fulani ya mawasiliano, then think twice.