Msaada wa kisheria kuhusu ndoa ya Mengi na K-Lynn


Mengi na K-Lynn wameweka picha za harusi yao jadharani. Hakuna aliyekiuka privacy. Katika convept ya privacy kina kitu kinaitwa "expectation of privacy". Ikipost picha zako instagram una void any expectation of privacy, kwa sababu umeweka picha katika public domain, watu wakianza kuzijadili huwezi kuwasema wasijadili kwani wanakuvunjia privacy.

Kama hili halina tija, mbona unalijadili?

Mengi kama mke wake wa kwanza alimuoa kwa ndoa isiyoruhusu kuongeza mke (katika cheti cha ndoa Tanzania kuna hiyo sehemu) na bado hajatoa talaka kwa mke wa kwanza, huyu wa pili ni movie tu.
 
kwa hiyo wale watoto sio wa Mengi kwa mujibu wa sheria ??
 

Tunaongelea POINT OF LAW which is a public concept!
 
watu mnabishana sana,duh...i believe no one is above the law,kama talaka ilishakubalika court basi klynn halali,if not then ni void lkn hata kama ni void haitamaanisha watoto wa klynn na mengi hawatafaidika,they have rights pia,yule ni baba yao and he has an obligation ya kuwatunza hata kama akifa kesho mali zake zitawatunza
 
Ndoa afunge mwingine kwa mapenzi yake na pesa yake....kukereketwa akereketwe mwingine...mmmmh !! We got a long way to go, long way......
 
Naomba unifahamishe nitasoma wapi sheria hizi za ndoa kama unavyoziongelea vya vifungu.

Soma sheria ya ndoa ya mwaka 1971 (Law of Marriage Act,1971) ndio sheria mama kuhusu masuala yote ya ndoa na hakuna ndoa yoyote itaitwa halali kama inapingana na kifungu kilichomo kwny hii sheria ndio maana nlipotoa hicho kifungu cha 9 kinaelezea maana ya ndoa na ukiendelea kifungu cha 10 na 11 kinaelezea ni ndoa za kimila au za kimila tu ndizo zinaruhusu mtu kuoa mke mwingne na tena lazima mke mkubwa aridhie km hatoridhia na ukaendlelea kufunga tu hiyo ndoa itakua haramu pia
 
mimi nashindwa kuelewa maisha binafsi ya Mengi yanamuhusu yeye mwenyewe na familia yake wakati mwingine tuweke hoja zenye faida kwa taifa.
 
mimi nashindwa kuelewa maisha binafsi ya Mengi yanamuhusu yeye mwenyewe na familia yake wakati mwingine tuweke hoja zenye faida kwa taifa.

Suala si maisha binafsi ya mtu bali hapa tulikuwa tunawekana wazi km hali ya namna hii ikimtokea ata mtu mwingne awe anajua pakuanzia na si hivyo unavyonadhi tumejikita kujadili maisha ya mtu bali hapa tumetumia km nyenzo ya kuuangalia ukweli ulipo kulingana na sheria za nchi zinavyo sema.

Na pia ata majaji mahakamani huamua kesi kwa kutumia maamuzi ya kesi zenye majina ya watu katika kesi zilizo mbele yao (precedence) hivyo kwa hili hakuna tatizo lolote
 

ukaona wa kumtolea mfano ni Mengi tuu ndani ya tanzania nzima hizi ni chuki binafsi unaweza kuweka mada hapa JF bila kumtaja mtu na ukapata sheria za nchi zinazovyosema na msaada wa kisheria pia.
 
ukaona wa kumtolea mfano ni Mengi tuu ndani ya tanzania nzima hizi ni chuki binafsi unaweza kuweka mada hapa JF bila kumtaja mtu na ukapata sheria za nchi zinazovyosema na msaada wa kisheria pia.

Mungu wa mbinguni anasemwa, Obama, Clinton, na wengine zaidi na wakuu kuliko Mengi wanasemwa, who is Mengi so far kuzidi hao?
 

Cheti ni kimoja tu ila kina nakala mbili moja ya mke moja ya mume.Kanisani.hawatoi cheti,ila kwa mfano wakatoliki kwenye cheti chako cha ukristo inajazwa tu ile nafasi ya ndoa kuwa umefunga ndoa
 
Wewe utakuwa umetumwa si bure, kuoa mwanamke wa pili wakati bado upo ndoani ya mwanzo nako ni kuvunja sheria ya nchi? Sema amekiuka maadili ya kanisa na si kuvunja sheria za nchi ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…