Msaada wa kisheria kuhusu ndoa ya Mengi na K-Lynn

Msaada wa kisheria kuhusu ndoa ya Mengi na K-Lynn

Sioni umuhimu wa kujadili hi post humu, kwanza inakiuka privacy ya mtu, na haileti mafundisho yoyote hapa, kwanza kumbuk mzee mengi ni msomi, na anamwanasheria wake bw michael ngalo, huyu ni mshaur wa maswala yote ya kisheria juu ya mzee na kampuni. Hakuna kilichovunjwa hapo, by the way naomba tujadili vitu vyenye tija kwa hili halituhusu.

Mengi na K-Lynn wameweka picha za harusi yao jadharani. Hakuna aliyekiuka privacy. Katika convept ya privacy kina kitu kinaitwa "expectation of privacy". Ikipost picha zako instagram una void any expectation of privacy, kwa sababu umeweka picha katika public domain, watu wakianza kuzijadili huwezi kuwasema wasijadili kwani wanakuvunjia privacy.

Kama hili halina tija, mbona unalijadili?

Mengi kama mke wake wa kwanza alimuoa kwa ndoa isiyoruhusu kuongeza mke (katika cheti cha ndoa Tanzania kuna hiyo sehemu) na bado hajatoa talaka kwa mke wa kwanza, huyu wa pili ni movie tu.
 
kwa hiyo wale watoto sio wa Mengi kwa mujibu wa sheria ??
 
Sioni umuhimu wa kujadili hi post humu, kwanza inakiuka privacy ya mtu, na haileti mafundisho yoyote hapa, kwanza kumbuk mzee mengi ni msomi, na anamwanasheria wake bw michael ngalo, huyu ni mshaur wa maswala yote ya kisheria juu ya mzee na kampuni. Hakuna kilichovunjwa hapo, by the way naomba tujadili vitu vyenye tija kwa hili halituhusu.

Tunaongelea POINT OF LAW which is a public concept!
 
watu mnabishana sana,duh...i believe no one is above the law,kama talaka ilishakubalika court basi klynn halali,if not then ni void lkn hata kama ni void haitamaanisha watoto wa klynn na mengi hawatafaidika,they have rights pia,yule ni baba yao and he has an obligation ya kuwatunza hata kama akifa kesho mali zake zitawatunza
 
Ndoa afunge mwingine kwa mapenzi yake na pesa yake....kukereketwa akereketwe mwingine...mmmmh !! We got a long way to go, long way......
 
Naomba unifahamishe nitasoma wapi sheria hizi za ndoa kama unavyoziongelea vya vifungu.

Soma sheria ya ndoa ya mwaka 1971 (Law of Marriage Act,1971) ndio sheria mama kuhusu masuala yote ya ndoa na hakuna ndoa yoyote itaitwa halali kama inapingana na kifungu kilichomo kwny hii sheria ndio maana nlipotoa hicho kifungu cha 9 kinaelezea maana ya ndoa na ukiendelea kifungu cha 10 na 11 kinaelezea ni ndoa za kimila au za kimila tu ndizo zinaruhusu mtu kuoa mke mwingne na tena lazima mke mkubwa aridhie km hatoridhia na ukaendlelea kufunga tu hiyo ndoa itakua haramu pia
 
mimi nashindwa kuelewa maisha binafsi ya Mengi yanamuhusu yeye mwenyewe na familia yake wakati mwingine tuweke hoja zenye faida kwa taifa.
 
mimi nashindwa kuelewa maisha binafsi ya Mengi yanamuhusu yeye mwenyewe na familia yake wakati mwingine tuweke hoja zenye faida kwa taifa.

Suala si maisha binafsi ya mtu bali hapa tulikuwa tunawekana wazi km hali ya namna hii ikimtokea ata mtu mwingne awe anajua pakuanzia na si hivyo unavyonadhi tumejikita kujadili maisha ya mtu bali hapa tumetumia km nyenzo ya kuuangalia ukweli ulipo kulingana na sheria za nchi zinavyo sema.

Na pia ata majaji mahakamani huamua kesi kwa kutumia maamuzi ya kesi zenye majina ya watu katika kesi zilizo mbele yao (precedence) hivyo kwa hili hakuna tatizo lolote
 
ukaona wa kumtolea mfano ni Mengi tuu ndani ya tanzania nzima hizi ni chuki binafsi unaweza kuweka mada hapa JF bila kumtaja mtu na ukapata sheria za nchi zinazovyosema na msaada wa kisheria pia.
 
ukaona wa kumtolea mfano ni Mengi tuu ndani ya tanzania nzima hizi ni chuki binafsi unaweza kuweka mada hapa JF bila kumtaja mtu na ukapata sheria za nchi zinazovyosema na msaada wa kisheria pia.

Mungu wa mbinguni anasemwa, Obama, Clinton, na wengine zaidi na wakuu kuliko Mengi wanasemwa, who is Mengi so far kuzidi hao?
 
Kwa uelewa wangu, ukifunga ndoa ya kikristo, unapewa vyeti viwili vya ndoa, cha serikali na cha kanisa. Kile cha serikali kina sehemu unaamua kama ni ndoa ya mke mmoja au zaidi ya mke mmoja. Yaani, ukichagua mke mmoja serikali nao wanasajili hivyo kuwa ulisaini mkataba huo kuwa wa mke mmoja na si vinginevyo...

Cheti ni kimoja tu ila kina nakala mbili moja ya mke moja ya mume.Kanisani.hawatoi cheti,ila kwa mfano wakatoliki kwenye cheti chako cha ukristo inajazwa tu ile nafasi ya ndoa kuwa umefunga ndoa
 
Ndoa ya leo ya Dr. Mengi na K-Lynn ni ya kweli? au ndio tusubiri siku Dr. Mengi ajekuita waandishi wa habari na kukanusha tena kuwa ni uvumi tuu?

Street is talking kwamba ndoa ya Dr. Mengi na mkewe Mercy is still valid (yani hawajatalikiana), kutokana na ukweli ya kwamba ndoa hiyo ilikuwa ni ya kanisa (until death do them apart). Sasa hapa ndipo ninapoomba msaada wa sheria katika maswali yafuatayo:-

1. Kama ni kweli ndoa ya kwanza haijatengulia, je Dr. Mengi atakuwa amevunja sheria ya inchi kufunga ndoa na K-Lynn hata kama ndoa imefungwa inchi nyingine?

2. Assume Dr. Mengi hakuweka wazi nani atakuwa muamuzi wake mkuu katika maswala ya afya. Je, kama ikatokea Dr. Mengi amepata matatizo ya kiafya na hawezi kufanya maamuzi muhimu, je inawezekana k-Lynn akawa na final say as it seems Dr. Mengi and his first wife doesn’t get along?

3. Kwakuwa K-Lynn anawatoto na Mr. Mengi, je hao watoto watakuwa part of Mengi’s estate hataka ndoa hiyo ikagundulika kuwa batili?

4. Kama mke mkubwa akajatambua kwamba kweli kuna ndoa imefungwa wakati yeye bado ana ndoa halali na Dr. Mengi, je, kisheria naruhusiwa kumfikisha Dr. mengi mahakamani na kumshitaki?

Naomba mtusaidie kujua atamshitaki kwa kutumia kipengele kipi cha sheria?

Asanteni!
Wewe utakuwa umetumwa si bure, kuoa mwanamke wa pili wakati bado upo ndoani ya mwanzo nako ni kuvunja sheria ya nchi? Sema amekiuka maadili ya kanisa na si kuvunja sheria za nchi ndugu
 
Back
Top Bottom