Msaada wa kisheria kuhusu PPF

LOVE U JF

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2015
Posts
2,138
Reaction score
1,639
Wanajamvi habari, kama maada inavyo tambulishwa, tumeajiliwa kwenye taasisi binafsi na tuliunganishwa na mfuko wa PPF (kabla mifuko haijaunganishwa ) cha ajabu wafanyakzi wanafukuzwa na ppf zao hupewa na taasisi na syo mfuko ,huko ppf ukienda kuuliza salio hakuna kitu je hapo wa kumshitaki ni mwajili asiye peleka pesa za wanachama au mwajili anayelipa nusu ya pesa yako tu ( ile % ambayo mwajili hukatwa) hyo hupewi katu!
Je kisheria hyo inakaa vipi?
Asanteni !!!
 
Kawashitaki mahakamani. Bodi ya PPF (now as PSSSF)iwe mshtakiwa na kwanza. na Mwajiri wako mshtakiwa wa pili.

Si jukumu la muajiriwa kumfuatilia muajiri wake kulipa michango. Ni kazi ya PPF (now as PSSSF). Ndio maana wa nguvu za kisheria kumshurutisha mwajiri alipe.
 
PPF wana kosa gani wakati inaonekana mwajiri hajapeleka michango PPF?
 
PPF wana kosa gani wakati inaonekana mwajiri hajapeleka michango PPF?
PSSSF wameshndwa kutekeleza majukumu yao kama sheria inavyowataka wafanye.
Ukisema ushitaki mwajiri tu itakuwa ngumu sana katika kutekeleza hukumu maana PSSSF ambaye hukusanya michango siyo sehemu ya hiyo kaza hukumu ya mahakama.
 
PPSSF anapokea na kutunza michango yako na kuhakikishwa utalipwa unapostaafu ni jukumu la mwajiri na mwajiriwa kuhakikisha michango inapelekwa ,Kama mwajiri atachelewa kupeleka michango Sheria inasema atapigwa faini na PPSSF
PSSSF wameshndwa kutekeleza majukumu yao kama sheria inavyowataka wafanye.
Ukisema ushitaki mwajiri tu itakuwa ngumu sana katika kutekeleza hukumu maana PSSSF ambaye hukusanya michango siyo sehemu ya hiyo kaza hukumu ya mahakama.
 
PPF wana kosa gani wakati inaonekana mwajiri hajapeleka michango PPF?
Mkuu kisheria yye ppf ndiye anatakiwa kumuwajibisha mwajiri maana mimi naona kama kuna mchezo wa kulindana kati ya mfuko na mwajili
 
Mkuu kisheria yye ppf ndiye anatakiwa kumuwajibisha mwajiri maana mimi naona kama kuna mchezo wa kulindana kati ya mfuko na mwajili
Yes but inachukua muda sana kuja kugundua hilo tatizo ,wafanyakazi wengi ni wazembe kufuatilia mambo yao wanasubiri mpaka matatizo yatokee ndio wanaamka.Sheria inasema auditor wa PPSSF atakuwa akigundua mchango haipelekwi ndio atamwandikia mwajiri sasa jiulize hiyo auditing huwa inafanyika baada ya muda gani ?

Kama unafanya kazi ni jukumu lako (mfanyakazi) kufuatilia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii kama michango yako inapelekwa kila mwezi.PPF wana (Android App,Website au option ya SMS) kuangalia michango yako, kama haipelekwi ndio unatoa taarifa PPSSF ili wafuatilia mapema sio una subiri hauko kazini miezi 6 imepita ndio unaanza kufuatilia
 
noted with thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…