Msaada wa Kisheria kuhusu Sheria ya Uzembe na Uzururaji

Piere. Fm

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
2,220
Reaction score
1,183
Samahani wakuu mimi ni mgeni katika Jukwaa hili, Naombe Msaada kuhusu sheria ya Uzembe na Uzururaji
ni kweli hii sheria ipo?
Na kama ipo inasemaje kuhusu Mazingira ambayo mtu anaweza kukamatwa Kama mzembe na mzurulaji?
Na je mpaka sasa sheria hii inafanya kazi?
Natanguliza shukrani.
 
Sheria hii ipo na inafanyakazi. Kwa mfano watu wanaoleta post zisizokuwa na mashiko kama hii yako, hushitakiwa kwa uzembe na uzuluraji!
 
Sheria hii ipo na inafanyakazi. Kwa mfano watu wanaoleta post zisizokuwa na mashiko kama hii yako, hushitakiwa kwa uzembe na uzuluraji!

Nashukuru kwa hilo KATALINA kwasababu nilikua sifahamu kuhusu hilo.
 
Hii sheria ipo sema application yake ni ngumu sana,nadhani ni kati ya sheria ambazo ziko kwenye sheria ya nguvu kazi:The human deployment act na kwenye penal code :rogue and vagabonds.Mfano mtu unamkamata mchana kuwa hafanyi kazi utatumia vigezo gani wakati labda yeye yuko night shift,au anatembea usiku saa 7 unasema ni mzurulaji kuna justification gani wakati nchi haina hali ya hatari ya kuzuia watu wasitembee usiku?ni kati ya sheria ambazo nadhani Nyalali alipendekeza zifutwe kwa vile hazina maana yoyote,ndio maana siku hizi ni nadra sana kukuta polisi wakifanya misako ya wazembe na wazurulaji.Naomba kuwasilisha tafadhali.
 
shukrani sana mkuu binafsi niliamua kuuliza hivyo kwasababu mwishon mwa mwaka jana nilishuhudia maeneo ya sumbawanga polisi wakiwakamata watu mida ya saa tatu usiku eti ni kwa kosa la uzembe nauzurulaji binasi nilishangaa na kushtuka and that why nikaamua kuipost hii kitu hapa ili niweze kupata uelewa kidogo. yote kwa yote nakshukuru sana mkuu kwa maelezo yako.
 
Ndio ipo,, ipo katika sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 177,. Wazembe na wazururaji. Kwanza nianze kuelekea kifungu cha 176 maana vinahisiana kwamba '176:" mtu yeyote akiwa ni muuza kilabu ya pombe, hoteli, bar , duka, chumba au mahali pengine panapofikiwa na watu mara kwa kwa ajili ya kununua au kunywa viburudisho vya namna yoyote, anaruhusu au kukubali kwa makusudi makahaba wa kawaida anyika na kuhaki katika jengo lake kwa kukusanyika na kubaki katika jengo lake kwa njia ya ukahaba, mtu huyo atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kwa adhabu ya isiyozidi shilingi mia tano au, iwapo ni kosa la mara ya pili na nakuendelea atatozwa faini isiyozidi shilingi elfu moja " hiki ni kifungu cha cha 176 niliona nikielezee kwanza maana kinahusiana na cha 177 kinachohusu uzembe na uzururaji :177 :Yeyote miongoni mwa watu wafuatao-
(a) mtu aliyepatikana na makosa kwa mujibu wa fungu la 176 baada ya kuwa alipata kuonekana kama ana makosa ya zamani ya kuwa mzėmbe na mzururaji;
(b) mtu atakayetangatanga kwa ukusanyaji sadaka au kujaribu kupata mchango au msaada wa namna yoyote ile kwa njia ya kujisingizia au hadaa
(c) mtu aliyetuhumiwa au mwizi mashuhuri amhaye hana njia zinazoonekana bayana za kupata maisha na hawezi kujieleza sawa sawa
(d) mtu anakayeonekana ndani au kwenye au karibu na nyumba popote hadhara yoyote au katika njia au barabara yoyote au mahali karibu na njia au barabara, au katika mahali pa hadhara katika wakati na hali ambayo yapelekea kana kwamba mtu huyo yupo hapo kwa jambo lisilo halali au la kikorofi
(e) mtu ambaye bila ya ruhusa ya maandishi ya Mkuu wa Wilaya au ikiwa ni manispali au mji, afisa mkuu wa polisi wa manispaa hiyo au mji huo, atakusanya au kuomba michango ya fedha ya jambo lolote katika mahali popote pa hadhara ndani ya wilaya hiyo, manispaa au mji huo atahesabiwa kuwa ni muhuni na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela , na kwa kila kosa litakalo fuata kifungo cha mwaka mmoja jela" ukiwa penal code utaisoma hapa pia hata kwenye kesi mashuhuri ya Jamhuri dhidi ya James Robert alikamatwa akiwa sehemu ya kununulia wanawake wanaojuhuza, mahakama ilisema James Robert alishikwa na hatia kwamba anakesi ya kujibu,, mahakama ilimtia hatiani James kwa kifungo cha nje miezi sita baada ya kujitetea kwamba alifaka pale kumfumania mpenzi wake,, kwa hiyo hiyo sheria ipo
Waalam jf members
 
Mkuu kwema! Nimekupm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…