Ndio ipo,, ipo katika sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 177,. Wazembe na wazururaji. Kwanza nianze kuelekea kifungu cha 176 maana vinahisiana kwamba '176:" mtu yeyote akiwa ni muuza kilabu ya pombe, hoteli, bar , duka, chumba au mahali pengine panapofikiwa na watu mara kwa kwa ajili ya kununua au kunywa viburudisho vya namna yoyote, anaruhusu au kukubali kwa makusudi makahaba wa kawaida anyika na kuhaki katika jengo lake kwa kukusanyika na kubaki katika jengo lake kwa njia ya ukahaba, mtu huyo atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kwa adhabu ya isiyozidi shilingi mia tano au, iwapo ni kosa la mara ya pili na nakuendelea atatozwa faini isiyozidi shilingi elfu moja " hiki ni kifungu cha cha 176 niliona nikielezee kwanza maana kinahusiana na cha 177 kinachohusu uzembe na uzururaji :177 :Yeyote miongoni mwa watu wafuatao-
(a) mtu aliyepatikana na makosa kwa mujibu wa fungu la 176 baada ya kuwa alipata kuonekana kama ana makosa ya zamani ya kuwa mzėmbe na mzururaji;
(b) mtu atakayetangatanga kwa ukusanyaji sadaka au kujaribu kupata mchango au msaada wa namna yoyote ile kwa njia ya kujisingizia au hadaa
(c) mtu aliyetuhumiwa au mwizi mashuhuri amhaye hana njia zinazoonekana bayana za kupata maisha na hawezi kujieleza sawa sawa
(d) mtu anakayeonekana ndani au kwenye au karibu na nyumba popote hadhara yoyote au katika njia au barabara yoyote au mahali karibu na njia au barabara, au katika mahali pa hadhara katika wakati na hali ambayo yapelekea kana kwamba mtu huyo yupo hapo kwa jambo lisilo halali au la kikorofi
(e) mtu ambaye bila ya ruhusa ya maandishi ya Mkuu wa Wilaya au ikiwa ni manispali au mji, afisa mkuu wa polisi wa manispaa hiyo au mji huo, atakusanya au kuomba michango ya fedha ya jambo lolote katika mahali popote pa hadhara ndani ya wilaya hiyo, manispaa au mji huo atahesabiwa kuwa ni muhuni na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela , na kwa kila kosa litakalo fuata kifungo cha mwaka mmoja jela" ukiwa penal code utaisoma hapa pia hata kwenye kesi mashuhuri ya Jamhuri dhidi ya James Robert alikamatwa akiwa sehemu ya kununulia wanawake wanaojuhuza, mahakama ilisema James Robert alishikwa na hatia kwamba anakesi ya kujibu,, mahakama ilimtia hatiani James kwa kifungo cha nje miezi sita baada ya kujitetea kwamba alifaka pale kumfumania mpenzi wake,, kwa hiyo hiyo sheria ipo
Waalam jf members