tanganyikakwanza
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 493
- 186
Kijana mmoja alikuja kuomba ushauri kwangu na haya ndiyo maelezo yake,anaomba ushauri kwa wanaoijua sheria.
Nawasilisha.
Mimi nilikuwa mmoja wa kundi la majambazi waliotingisha sana nchi na kuiba bila kujulikana lakini kutokana na ugomvi uliotokea kwenye kundi memba wa squad wenzangu wakanitimua lakini nimekaa mwaka mzima sijawahi kumwambia mtu na katika huo ujambazi tulikuwa tukiua.
Sasa nataka baada ya kundi hilo kudai mimi nilittaka kulipua gari lao ili wafe nikaona niitishe waandishi wa habari na kwenda msikitini kutubu.
Sasa msaada ninoomba
- Je,polisi wataniita kama shahidi kwa sababu nimekiri au nitakuwa mtuhumiwa?
- Je nitatakiwa kuishi Segerea au nyumbani kipindi chote cha kesi?
- Je na kama nikishindwa kutoa ushahidi usio na shaka kuhusu memba wenzangu kesi itafutwa au watanishikilia mimi niliyekiri tayari?
Nawasilisha.