Msaada wa kisheria kuugua ukiwa kazini?

Msaada wa kisheria kuugua ukiwa kazini?

Roga Roga

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
656
Reaction score
499
Ndugu wadau wa Jf naomba mniweke sawa hasa katika masuala ya kisheria kwa mtumishi wa uma anapopata matatizo ya kiafya akiwa kazini.

Nina mdogo wangu ameajiriwa halimashauri ya Masasi, Mtwara, tangu mwaka jana mwishoni amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya, ametibiwa huko Masasi bila mafanikio na kupewa rufaa kuja hospitali ya mkoa ya Ligula mtwara. Hapa hospitali ya rufaa bado hakupata nafuu yoyote na hivyo kupewa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajiri ya uchunguzi zaidi.

Tangu akiwa Masasi baadae kuja mtwara na kuelekea hospitali ya Muhimbili hakuna msaada wowote wa kifedha kwaajiri ya safari,chakula na pakulala ameupata toka kwa mkurugenzi wa masasi ambaye ni muajiri wake. Muda aliotumia Muhimbili ni mwezi mmoja na nusu. Baada ya kupata nafuu, amerejea kazini tangu mwezi march mwaka huu na pia akachukua jukumu la kuomba arudishiwe gharama zote alizotumia katika matibabu ikiwemo safari,chakula na gesti.

Pia kama mjuavyo hospitali nyingi za serikali hazina vipimo vya kueleweka,na wakati mwingine ilimlazimu kutumia fedha yake kwenda kufanya vipimo katika hospitali binafsi ili kuokoa maisha yake. Viambata vyote vya tiketi, matibabu,vipimo amewasilisha lakini mpaka leo hajarudishiwa gharama hizo. Je ni sheria ipi ya kazi inaweza kumlinda na hatimaye kufidiwa? Ikumbukwe matatizo yake yamepatikana akiwa kazini? Na sasa baada ya kufatilia muda mrefu wanamtishia kumfuta kazi.

Msaada wenu ni muhimu.
 
Amejibiwa vipi baada ya kuomba kurejeshewa gharama alizotumia?
Je hakuna fedha,hakufuata taratibu au mkurugenzi kakataa?
 
Amejibiwa vipi baada ya kuomba kurejeshewa gharama alizotumia?
Je hakuna fedha,hakufuata taratibu au mkurugenzi kakataa?

Utaratibu wote ameufuata ikiwepo kuomba ruhusa kila aliposafiri na alikuwa akiambatanisha nakala za hospitali muda wote. Ameandika barua zaidi ya nne lakini mpaka leo hajajibiwa chochote
 
Kama Kuna Kikundi Cha Wafanyakazi Amejiunga Nacho Aende Akaelezee Shida Yake Watamsaidia, ,pia Aweza Kwenda Kufungua Mashtaka Bodi Inaitwa CMA, ,
Ingekua Vizuri Kama Ungetafta Mwanasheria Mwongee Ana Kwa Ana Usaidiwe Kirahisi Na Kwa Ufanisi
 
duu ameajiriwa taasisi ya serikali au private,ana haki ya kurudishiwa pesa zake za matibabu,kumfukuza kazi ni kumuonea,chama cha wafanyakazi kitaweza kumsaidia
 
Kama Kuna Kikundi Cha Wafanyakazi Amejiunga Nacho Aende Akaelezee Shida Yake Watamsaidia, ,pia Aweza Kwenda Kufungua Mashtaka Bodi Inaitwa CMA, ,
Ingekua Vizuri Kama Ungetafta Mwanasheria Mwongee Ana Kwa Ana Usaidiwe Kirahisi Na Kwa Ufanisi

Asante kwa msaada wa kimawazo.
 
Back
Top Bottom