Msaada wa kisheria kwenye bima

Msaada wa kisheria kwenye bima

kyemo

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2010
Posts
570
Reaction score
718
Habari zenu wadau!Natafuta msaada wa kisheria katika masuala ya bima.Nahitaji kufungua kesi kuishitaki kampuni moja ya bima kwa kutolipa madai yangu na kukaa kimya bila kujibu madai yangu,tatizo nimeenda law firm moja wanataka hela ambayo ni nyingi kwangu kwa sasa,naomba mwenye uelewa wa masuala ya kisheria tuwasiliane jinsi ya kusolve hii inshu coz tutaelewana kabla,naamini hii kesi nitashinda.
 
Pole sana! Kabla ya yote jaribu kupitia vizuri policy ambayo ni contract kati yako na hiyo kampuni ili ujiridhishe vizuri.. Mara nyingi makampuni ya bima yanajua sana kucheza na terms and condition ktk policy ili kukwepa madai.
 
mkuu ungeliweka jina la kampuni lingesaidia kutoa taadhari kwa wengine ili kufanya maamuzi mazuri wakati wanataka kukata bima.Pia kwa upande wako ingelikuwa bora ungeliweka na kosa lako tujui tunakushauri vipi
 
Habari zenu wadau!Natafuta msaada wa kisheria katika masuala ya bima.Nahitaji kufungua kesi kuishitaki kampuni moja ya bima kwa kutolipa madai yangu na kukaa kimya bila kujibu madai yangu,tatizo nimeenda law firm moja wanataka hela ambayo ni nyingi kwangu kwa sasa,naomba mwenye uelewa wa masuala ya kisheria tuwasiliane jinsi ya kusolve hii inshu coz tutaelewana kabla,naamini hii kesi nitashinda.

Unadai nini? Umeambatanisha nyaraka zipi kama msingi wa madai yako? Unawapeleka mahakamani kwa basis ipi?
 
Jina ni Mwananchi Insurance company,nimeshafata procedure zote hadi kwa regulator ambao ndio wamenishauri nitafute msaada wa kisheria
 
Bima wanazingua sana asee,,mi pia kuna jamaa yangu alishafata process zote na mwisho wa siku wakamwambia wanaprocess malipo,,ss ishapita zaid ya miez 6 amna malipo wanazungusha tuu
 
Back
Top Bottom