Kuna Professa Mmoja (Jina namhifadhi) ambaye alifariki Dunia 2012. Kaacha Majanga kwa watoto wake kwa Sababu hakuandika wosia kabisa. Huyo Mzee tumsamehe tu lakini nachoomba ni ushauri tu kwa wataalamu wa Sheria.
Huyu Professa alioa mwaka 1984 na mke wa kwanza ni mzungu na akazaa naye watoto wawili.(Mtoto Wa kwanza ni wa kiume wa na Mtoto wa pili ni wa kike) na waliishi hapa Dar na Wakajenga Nyumba Mikocheni na kununua Magari na Kiwanja. Sasa kwenye miaka 1990 walipeana talaka na waliachana na huyu Mzungu mwanamke akarudi kwao ulaya.
Professa alibaki dar na mali zote pamoja na watoto wake na aliwasomesha watoto wake hadi elimu ya chuo.
Sasa huyu professa alikuja kuoa tena mwanamke mwingine 2005 na alizaa naye Mtoto mmoja wa kike. Huyo Professa alinunua kiwanja na alimjengea mke wake wa pili, nyumba, shamba na vilevile alimnunulia gari la kutembelea.
Sasa professa alipofariki Dunia 2012. Watoto wake walikuwa bado wanasoma chuo Nje ya Nchi. Yule Mama aliteka mali zote kuanzia viwanja, Nyumba, Magari, Pesa kila kitu kachukua. na ameshafungua kesi Mahakama kuu anataka kibali cha kusimamia Mirathi. Hio kesi bado haijaisha ipo mahakamani mwaka mzima sasa na inaelekea ushindi upo kwa yule mama. (Mke wa pili)
Wale watoto wa marehemu wamerudi Dar hawana chochote hawana mahali pa kukaa, wanakaa kwa ndugu zao. wanapata shida kweli. Yule Mama wa kambo anaendelea kutesa tu na magari ya Professa.
Ndugu wamejaribu kuwapigania kesi hawa watoto lakini wanakwama kwa sababu yule Mama wa kambo kahonga pesa kila sehemu na Ushindi unaelekea kwake. Marehemu Hakuacha wosia kabisa. Naomba ushauri wa kisheria. Hawa Watoto wake wa kwanza watapata haki zao kweli?