Msaada wa kisheria kwenye suala la bima

Msaada wa kisheria kwenye suala la bima

Tingitane

Senior Member
Joined
Apr 18, 2012
Posts
116
Reaction score
132
Habar za humu wakuu,

Naomba msaada wa kisheria kuhusu tatizo linalonisumbua.Ni hivi mnamo mwaka 2018 mwezi wa sita nillipata ajali ya gari ikihusisha gari yangu na niliendesha mwenyewe na gari yakampuni moja ya usafirishaji wa abiria jijni Dar es salaam almaarufu kam ......

Traffic alikuja na kupima ajali na akaamuru gari yangu ipelekwe kituo cha police maana iliharibika sna na baada ya taratibu zote za kipolisi ilionekana mwenye kosa ni dereva mwezangu na hivyo kesi ikapelekwa mahakamani na mahakama ikaamua dereva mwenzangu alipe faini.

Nikaaanza kufatilia malipo ya gari yangu kupitia bima ya aliesababisha ajali kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa pale polisi lakini baadae niligundua kuwa bima yao haikuwa hai na kampuni husika wakaniambia hawawezi kunilipa.

Nikairudia ile kampuni wakaonesha kwamba wameweka sawa na bima nitalipwa lakin mwisho wa siku nikagundua nahangaishwa tu na nikahamishwa kikazi hapo dar es salaam hivyo uwezekano wa kufuatilia ukawa mdogo zaidi. Ninaomba yeyote mwenye ushauri wa kisheria anisaidie kwani gari iliharibika sana"total loss"na imelala garage mpaka leo.

Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom