Kwa sheria ya dini ya kiislaam...
Mtu harithiwi mpaka afe(awe maiti)
Kabla ya kifo huo ni wosia...
Na wosia hauandikwi juu ya wale wenye haki ya kurithi...
Na wenye haki ya kurithi ni mama, baba, mke, mume watoto, na kaka na dada. ..wa marehemu
Na wosia hautakiwi kuzidi theluthi ya mali nzima ya marehemu...
Na mirathi inahusu mali ya marehemu tu ukiondoa kile alichousia au deni...
Mali ni yako uliyochuma mwenyewe tu...
Hakuna mali ya pamoja kama hamkuchuma pamoja... Iwe kabla ya ndoa au baada ya ndoa. .. Iwe ya mke au mume...
Mali inayogawiwa mirathi iwe ndogo au kubwa. ..
Kisheria ya kiislaam. .. Mirathi imeshagawiwa na allah. .. Hakuna anayeruhusiwa kugawa mirathi tofauti na alivyogawa allah. .. Kinyume chake ni dhambi kubwa kwenda kinyume na sheria ya allah. ..
Ahsante.. .