Msaada wa kisheria, nataka kuishtaki serikali kwa matumizi mabaya ya kodi

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
2,026
Reaction score
3,107
Ambonyi,

Kufuatia tukio lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo tulishuhudia Polisi wakitumia gharama kubwa kumkamata na kumsafirisha Tundu Lissu kutoka Singida mpaka Dar kwa ajili ya kuhudhuria kesi yake aliyofunguliwa na Jamuhuri. Kama mzalendo nimeguswa sana na namna ambavyo Jeshi la Polisi limetumia vibaya kodi ya wananchi wanyonge kufanya kitu ambacho mwisho wake hakikuwa na tija kwa taifa.

Ukifanya simple analysis kwa kuangalia:

1. Idadi ya polisi waliotumika,
2. Garama za maisha kwa siku mbili kwa polisi na mtuhumiwa wao
3. Garama za magari yaliyotumika katika msafara wa siku mbili
4. Garama za mawasiliano, ngazi zote Wakati wote wa kulifuatilia tukio
5. Garama za mawakili wa jamuhuri, ambapo walibwagwa na mtuhumiwa katika hatua ya kwanza
6. Usumbufu wa kisaikolojia wa wananchi na viongozi wao kwa kipindi chote cha saga la Lissu

Kwa kweli ni garama kubwa sana, ukizingatia inatokana na kodi za wananchi wanyonge, hela hii ingeweza kutumika kufanya mengi na ya maana kwa wananchi Kama: kununua madawa, madawati, vitanda nk.

Naomba mwongozo wa namna ya kufile kesi hii toka kwa wajuzi wa haya mambo ya sheria.
 
safi sana mkuu, ningekuwa mwanasheria ningekusuport, ila kila la heri
 
Kabla haujaishtaki hakikisha unavigezo hivi:
1)Locus Stand(interest):kwa maana unamaslahi yoyote katika kiini cha kesi aidha maslahi binafsi au unamaslahi kwa niaba ya Watanzania.

2) Unapotaka kuishtaki Serikali hususan serikali kuu lazima ufuate taratibu za Government Proceedings Act No 05[re 2002].miongoni mwa taratibu hizo ni kuijulisha idara husika ya serikali unayoishtaki kwa kuandika notisi ya siku 90 kwa idara au wizara husika,zaidi pitia sheria hiyo ujue taratibu nyinginezo.

3)Usikurupuke.
 
Back
Top Bottom