Pole kwa mkasa uliokufika.
Mimi si mwanasheria lakini hatua ya kwanza unayopaswa kuichukua ni kutafuta Jedwali la Polisi Na. 3 yaani PF3 iwapo ulipelekwa hospitali na ripoti ya daktari ambapo ulitibiwa. Kama hutopata PF3 basi ripoti ya polisi inatosha.
Kutegemea na mkoa ambao unaishi, tafuta tawi la asasi inayotoa msaada wa kisheria, NOLA au nenda kwenye Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Kibinadamu, yaani Legal and Human Rights Centre.
Watu wengi hukamatwa na polisi, kwa kuwa hawajui haki zao, hupigwa na kuteswa, kisha hulazimishwa kuandika maelezo ya uongo kabla ya kuachiwa. Nimeshuhudia hili.
Usiogope lakini jiandae kwa changamoto. Andika maelezo yako yote kwa umakini. Taja majina ya wahusika wote. Kama kuna mashahidi ni vizuri uwajumuishe na kuwashirikisha. Shahidi ni mtu ambaye alishuhudia ulivyoteswa, iwe ni kabla, wakati wa, au baada ya. Kwa mfano, kama kuna mtu alikusaidia kukupeleka hospitali, huyo ni shahidi japokuwa hakuwepo wakati unapigwa. Ni shahidi kwa kuwa anajua kwamba ulipigwa na alikupeleka hospitali.
Kila la heri.