Msaada wa kisheria: Partnership kwenye biashara

Tuttyfruity

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2017
Posts
2,414
Reaction score
6,371
Habarini wana jamvi. Nimeamua kuja hapa kuomba ushauri kwa hili swala. Nimeona nije kwa watu wasionifahamu ili kuondoa "conflict of interest"

Straight kwenye mada, kuna biashara nimekua nikifanya kwa muda wa mwaka mmoja sasa. Nilianza from scratch mwenyewe bila msaada kutoka kwa mtu yeyote. Okay alhamdulilah one year down the line biashara imekua , na ina potential ya kukua zaidi. Yani inshort si meet demand ya wateja kwa sababu nna limited funds.

Unajua tena ukianza kufanya kitu watu huwa wanakucheki tu kuona how far you will go with it.

okay nisiwe muongo I want to bring all the facts ili mnipe ushauri mzuri, kuna jamaa nilikua natoka nae sawa, katika mapenzi yetu tulivyokua tuna share mambo yetu akawa intrested na biashara yangu, jinsi nnavyoifanya na faida nnayoitengeneza alivutiwa ku invest lkn katika mda ule alikua na mambo mengi hakuweza. Sasa tumeachana na huyu jamaa lakini karudi anataka ku invest . For my own safety nimemwambia a invest the same amount that my business is worth ili asinizidi kete.

tatizo liko hapa, although huyu jamaa ana invest fedha lakini management na operations zote ntakua nafanya mimi. It's an online business currently I run all social media, Facebook, Instagram, WhatsApp business etc. na kama mnavojua online business haina muda wa kufunga yani nakua online muda wote. Nashughulikia logistics kuorder, kusafirisha mpaka kupokea mzigo ni mimi. Sales na deliveries nafanya mimi na ntaendelea nafanya mimi cause this guy yeye anaishi mji mwingine.

shida inakuja hapa, huyu jamaa anataka tugawane profit 50,50. Nimefikiria mimi ndo ntakua ninafanya kazi zote muda wote it is unfair kugawana faida sawa bin sawa.

secondly kuna mtu nimemuuliza kaniambia kama mimi ndo ntakua nna run hiyo biashara full time ikitokea huko mbeleni tukapata hasara basi jamaa anaweza kunibana nimlipe pesa yake + profit. Sijajua hili lina ukweli kiasi gani. Lakini hiki kimenifanya niogope.

mimi nataka tugawane 60% by 40% profit kwa sababu nlizozitaja hapo.
Also jamaa anataka ku draft some kind of legal paper work which will legally bind me in the contract. Sitaki ku sign kitu kitakacho niweka matatizoni baadae au hata kupotezq biashara yangu kabisa cause this is all I got.

Guys nipeni ushauri unaoeleweka, ushauri ulioenda shule. Kama kuna lawyers humu ndani itakua vizuri zaidi.

msiuseme muandiko wangu hakuna alionilipia ada humu ndani.

Wsalaam.
 
Unapokuwa unafanya kazi then upigie mahesabu kiasi cha pesa unachopaswa kujilipa. Na iwe ni sehemu ya matumizi katika uendeshaji.

Kisha faida halisi ndiyo mgawane 50/50.
This is another problem, sijui natakiwa nijilipe kiasi gani.... au nipe % unayoona inafaa mimi kujilipa.
 
kuna kitu kinaitwa partnership deed(nadhani ndiyo hayo uliyosema ma legal docs jamaa anaandika).unachatakiwa kufanya ni kujuanni kwa kiasi gani utafaidika zaidi kwenye partneship kuliko kuwa sole propriator.Kama unaongeza chochote basi ingia kwenye hiyo partnership.sasa wakati wa kuweka mtaji wako wewe utaongeza na kitu kinaitwa goodwil,maana tayari wewe umeshatengeneza reputation kwenye business.kingine mkubalinea mshahra wa msimamizi,ambaye utakuwa ni wewe.kuhusu kugawana faidi inaweza kuwa 50/50 ikiwa muda wako unaotumia unafidiwa ipasavyo.nadhani mnatakiwa mtafute mwanasheria awatengenezee hiyo doc.

Muweke jamaa wazi risk zote zinazoiface hiyo biashara ili anapofanya maamuzi basi aelewe kwamba ikipatikana hasara nayo pia mtagawana hivyo hivyo(itapunguza mitaji yenu)

Ila umesound kama huyo jamaa alishawahi kuwa ni ex wako? kama ni hivyo kina la ziada kidogo
 
Kama ni mumeo, sawa. Ila kama ni mpenzi, jiandae kwa lolote.
Ni ex.... I'm trying to get more funds to grow my business but at the same time sitaki kujiingiza kwenye situation itakayo ni cost hapo baadae.
 
nimekwepa kusoma coment za wengine kukwepa wasije kunitoa kwenye point....point yangu ni kwamba....ume sema biashara inaenda vizuri!na huyo jamaa haupo naye kimapenz kwa sasa na kama biashara inaenda vizur unatak partinership ya nn tena?....pia huyo jamaa kuwa nae makin wenda anatafuta njia ya kukuporomoa ili akutawale ndo mrudiane vizuri....nime andik nimelewa lkn hta ningekuwa timamu intetion yangu inge bak hivihivi.....heri ya x mass n new year
 
This is another problem, sijui natakiwa nijilipe kiasi gani.... au nipe % unayoona inafaa mimi kujilipa.
Tumia mfano ufuatao. Assume hiyo biashara ingekuwa ni yangu kwa 100%, na kwa status hiyo hiyo uliyonayo sasa hivi, naamua kukuajiri unifanyie yale yote unayofanya sasa kwenye hiyo biashara, kwa muda wote ambao unafanya sasa!

Je, ungependa nikulipe Sh. ngapi kwa mwezi?

Baada ya hapo, tutaende sehemu ya pili kwa sababu suala sio tu ku-finance hiyo biashara ni lazima mkubaliane rasmi na sio kimapenzi namna ya ku-share Profit and Loss ili asije akawa anadai faida tu kwa sababu anaona biashara inatengeneza faida. Kwa kifupi, kuna mengi ya kuangalia!
 
Katika hizi biashara za ushirikiano (Partnership) kuna kuna mwongozo "Partnership Deed” ambao kwa kawaida huwa mnakubaliana mambo mbali mbali kama vile:
1. Jina la biashara
2. Aina ya biashara mtakazofanya
3. Kiwango cha mtaji kwa kila mmoja wenu kuchangia na hii ndio hutoa kiasi cha pesa za gharama kama vile kodi ya mapato kulipa, gharama za uendeshaji nk
4. Malipo kwa msimamizi/mfanyakazi/gharama za uendeshaji biashara yatalipwa vp kama kutoka ktk faida au kuwa 'partners' nk

Sasa kama hamkuwa na makubaliano yoyote bhasi mwenzio anatumia udhaifu huo kujinufaisha. Anyway, mwambie mrudi mezani mjadili mambo ya msingi kwa msaada wa mwanasheria awape mwongozo wa "Terms muhimu za Partnership Deed”!
Nawasilisha
 
Okay this makes sense.... that's why niliamua kulileta humu. So malipo naweza kuweka kwa % ?? So that as the business grows my salary grows as well right?
 

ahsante kwa mchango wako. Number 1-3 vipo wazi. Number 4 ndo nikijaribu kulileta mezani anasema yeye anataka faida ya 50% regardless. He even suggested kama he can invest more money ili tu apate faida ya 50%.

hatuna makubaliano yoyote ya kimaandishi although pesa ameshanikabidhi lakini bado sijaiingizw kwenye biashara. Deed of partnership amesema he will come up with it.

he's a smart man na pia ana tumia udhaifu wangu in his advantage. Akiongelea biashara anaingiza na story za kuzaa pamoja etc 😂😂 sijui we are going to be partners for life wakati ana girlfriend. I know he's saying all this to destruct me. I don't want to say no his offer cause hela naitaka pia lkn pia I want to secure my business and my future. Naamini hii biashara itakua kubwa sana na yeye ameliona hilo ndo mana he wants in.
 
Thing is hataki tutafute lawyer, he wants to do everything himself mimi ni sign tu... does it makes sense?
 
I have an idea nilipwe sh ngap, twende sehemu ya pili...
 
Kuna kitu kinaitwa "sweat compesation". Hata kama mkiwa na hisa sawa ila yule anayefanya "day to day activities" anakua na fungu lake tofauti na yule aliyetoa mtaji tu
 
Kwa maelezo yako ni kuwa huyu jamaa yeye ni mwekezaji na sio mshiriki wa biashara. Kilichopo ni kuw ntaka kuwekea pesa yake then mwisho wa siku faida mgawane sawa. Hili sijaona kama tatizo bali kuna masuala haya muweke wazi:

1. Uhusiano wenu hauna na hautambuliki na biashara ie business entity hvy mnapojadili suala la biashara either uwe na mwanasheria au Business Consultant ambae ataweka vema terms zenu za biashara. Huo mkataba akija nao lazima muujadili na vema ukishirikisha wengine ie wataalam

2. Gharama za uendeshaji biashara lazima ziwekwe wazi ili baada ya kufanyika biashara, yafanyike mahesabu ikibidi mtumie mhasibu ambae atawafanyia na kuweka wazi kila kitu na hatimae kugawana faida

3. Suala la kutumia muda wako mwingi ktk biashara hy, ndiyo ajira yenyewe, hence lazima ulipwe mshahara ambao mtakubaliana. Kumbuka hata huu mshahara ni sehemu ya gharama ya biashara kama ilivyo kodi, umeme maji et al
 
Okay this makes sense.... that's why niliamua kulileta humu. So malipo naweza kuweka kwa % ?? So that as the business grows my salary grows as well right?
Huwezi kuweka kwa asilimia bali basic salary ndiyo tunayolipana. Lakin ukiacha base salary, hapo utaweka gharama ya vitu vyote vinavyoendesha maisha yako binafsi na hatimae kukuwezesha kufanya biashara yenu bila stress. Kwa mfano, Rent Allowance na kingine chochote. Pamoja na Rent Allowance, lazima mkubaliane Bonus in case biashara inafanya vizuri lakini na wewe ili kuwa fair, mnatakiwa ku-define nini maana ya biashara kufanya vizuri! Kwa mfano, tuseme wakati mnaanza total mnaweka 10M, na mwisho wa mwaka mmeingiza 2M kama faida. Je, hiyo 2M kwa mwaka ndo biashara kufanya vizuri?! Ili usionekane you're too greed, angalia uhalisia wa kibiashara kwamba endapo ndo ungekuwa alone na mtaji ukapanda from nowhere to 10M, je unadhani kwa mwaka ungepata faida kiasi gani!

UKisema usingekosa 5M, lakini mkapata 7M, hapo biashara imefanya vizuri kwa sababu ime-exceed malengo lakini kama umepata hiyo hiyo 5M au 4M, sawa mmepata faida lakini hamja-exceed malengo kwahiyo hapo imefanya kawaida na hivyo imewapa kile kile ambacho kila mfanyabiashara anakitafuta; yaani faida!! Hii bonus ndo iwe kwa viwango vya %.

Hata hivyo, suala la mshahara liwe second option endapo mtashindwa kukubaliana suala la wewe kuchukua zaidi ya 50% ya faida (yaani kama ulivyosema hiyo 60%) na endapo unadhani unahitaji sana capital yake. Jitahidi kujenga hoja kwanza kwanini unaona ni muhimu kuchukua 60% kwamba % itaku-motivate zaidi kwa sababu unajua the more the profit you make ndipo unapopata zaidi!!!

Na lingine muhimu zaidi make sure business operations zinakuwa fully under your control; na hilo lisiwe na mjadala!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…