Msaada wa kisheria: Partnership kwenye biashara

Msaada wa kisheria: Partnership kwenye biashara

Habarini wana jamvi. Nimeamua kuja hapa kuomba ushauri kwa hili swala. Nimeona nije kwa watu wasionifahamu ili kuondoa "conflict of interest"

Straight kwenye mada, kuna biashara nimekua nikifanya kwa muda wa mwaka mmoja sasa. Nilianza from scratch mwenyewe bila msaada kutoka kwa mtu yeyote. Okay alhamdulilah one year down the line biashara imekua , na ina potential ya kukua zaidi. Yani inshort si meet demand ya wateja kwa sababu nna limited funds.

Unajua tena ukianza kufanya kitu watu huwa wanakucheki tu kuona how far you will go with it.

okay nisiwe muongo I want to bring all the facts ili mnipe ushauri mzuri, kuna jamaa nilikua natoka nae sawa, katika mapenzi yetu tulivyokua tuna share mambo yetu akawa intrested na biashara yangu, jinsi nnavyoifanya na faida nnayoitengeneza alivutiwa ku invest lkn katika mda ule alikua na mambo mengi hakuweza. Sasa tumeachana na huyu jamaa lakini karudi anataka ku invest . For my own safety nimemwambia a invest the same amount that my business is worth ili asinizidi kete.

tatizo liko hapa, although huyu jamaa ana invest fedha lakini management na operations zote ntakua nafanya mimi. It's an online business currently I run all social media, Facebook, Instagram, WhatsApp business etc. na kama mnavojua online business haina muda wa kufunga yani nakua online muda wote. Nashughulikia logistics kuorder, kusafirisha mpaka kupokea mzigo ni mimi. Sales na deliveries nafanya mimi na ntaendelea nafanya mimi cause this guy yeye anaishi mji mwingine.

shida inakuja hapa, huyu jamaa anataka tugawane profit 50,50. Nimefikiria mimi ndo ntakua ninafanya kazi zote muda wote it is unfair kugawana faida sawa bin sawa.

secondly kuna mtu nimemuuliza kaniambia kama mimi ndo ntakua nna run hiyo biashara full time ikitokea huko mbeleni tukapata hasara basi jamaa anaweza kunibana nimlipe pesa yake + profit. Sijajua hili lina ukweli kiasi gani. Lakini hiki kimenifanya niogope.

mimi nataka tugawane 60% by 40% profit kwa sababu nlizozitaja hapo.
Also jamaa anataka ku draft some kind of legal paper work which will legally bind me in the contract. Sitaki ku sign kitu kitakacho niweka matatizoni baadae au hata kupotezq biashara yangu kabisa cause this is all I got.

Guys nipeni ushauri unaoeleweka, ushauri ulioenda shule. Kama kuna lawyers humu ndani itakua vizuri zaidi.

msiuseme muandiko wangu hakuna alionilipia ada humu ndani.

Wsalaam.
Kama anaweka pesa kwa 50 % basi ujue faidi ni nusu kwa nusu ndiyo taratibu na kanuni za ubia, ila unachosema kama operation unazifanya wewe unatakiwa muweke mambo sawa, ni either hiyo kazi unayoifanya iwe ni kama ajira nje ya ubia wako, yani uwe unajilipa mshahara
 
KWA HUDUMA

KUSAJIL KAMPUNI
-jina la Biashara
-limited caompany
-partneship

HESABU ZA KAMPUNI(FINANCIAL STATEMENTS)

KUANDIKA MEMORANDUM

USAFI WA:
-Majumbani
-Viwandani
-maofisini
-hosipitalini
-shuleni
-maeneo ya jamii

TUKO NA UZOEFU WAKUTOSHA

Wasiliana nasi kwa # 0788104228

USHAURI NI BURE

Popote ulipo TANZANIA tunakupa huduma.
Klin&Brite
Nakuuliza swali nione ubobezi wako, kama una mubia asieishi Tanzania yani sio mtanzania ni lazima awe na TIN na anaiombaje yupo nje ya nchi
 
Hatimae amepigwa.

Nikionaga mtu anatafuta back up kwa waganga sijui namuonaje
 
Back
Top Bottom