Msaada wa kisheria plz kwa anayejua...

P I M

Senior Member
Joined
Feb 16, 2011
Posts
139
Reaction score
24
Jamaa alioa mke na kufunga nae ndoa (ya imani ya kiislam) japo haikudumu sana ingawa walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume na wakapeana taraka kila mtu akaendelea na maisha yake huku mwanamke akipata bwana mwngne na mme kuchukua mke (mkristo) mwngne na kuendeleza nae maisha na kufanikiwa kupata watoto watatu japo hawakuwahi kufunga ndoa ingawa wameishi pamoja kwa miaka 13 sasa.
Kwa maisha aliyoishi na huyu wa pili walifanikiwa kununua kiwanja na kujenga nyumba japo ujenzi wake haujakamilika.
Bahati mbaya jamaa ameisha fariki (kama miezi mitano imepita tangu afariki), hivi sasa kumeibuka mgogoro wa kifamilia kati ya wake zake wote japo yule wa kwanza walishapeana taraka na huyu wa pili hawakufanikiwa kufunga ndoa kwa miaka hiyo yote walioishi pamoja.
Sasa yule mke mkubwa kaenda mahakamani kudai mali alizoziacha mtaraka wake kuwa mwanae ndo mwenye haki na mali zile zote kwani hawa watoto hawana haki ya kumiliki chochote kwa 7bu baba yao hakuwahi kufunga ndoa na mama yao.
Kwa sasa kesi ipo mahakamani na mahakama imezuia uendelezaji wa aina yoyote kwny jengo/nyumba aliyoicha marehemu.

Je, kisheria nani mwenye haki wa umiliki wa mali za marehemu?
 
Huyu mke wa pili ndio mwenye haki ila haki yake si kama ya mke bali kama mtu "anayedhaniwa kuwa mke kwa dhana ya section 160 ya sheria ya ndoa.
 
Huyu mke wa pili ndio mwenye haki ila haki yake si kama ya mke bali kama mtu "anayedhaniwa kuwa mke kwa dhana ya section 160 ya sheria ya ndoa.

Na yule mtoto wa mke wa kwanza ana haki yoyote ya kupata urithi wowote kwenye mali za marehemu ukizingatia kuwa mama yake alishapewa taraka siku nyingi hata kabla ya baba yake kupata chochote?
 
Yah mtoto wa kwanza ana haki kikamilifu kbsa kwasababu alizaliwa katika ndoa halali. Hapo watoto wote wana haki yule wa ndoa ya kwanza na hawa wa mama wa pili, lakini je? Mna uhakika marehemu hajaacha wosia?
 
Na yule mtoto wa mke wa kwanza ana haki yoyote ya kupata urithi wowote kwenye mali za marehemu ukizingatia kuwa mama yake alishapewa taraka siku nyingi hata kabla ya baba yake kupata chochote?
ndio anayo
 
Huyu mke wa pili ndio mwenye haki ila haki yake si kama ya mke bali kama mtu "anayedhaniwa kuwa mke kwa dhana ya section 160 ya sheria ya ndoa.

Uko sahihi, lakini: 1. Kama marehemu alikuwa ana-confess Islam strictly, mali zake zitakuwa administered according to Islamic rules. Mkristo anaweza kudai haki ya jasho lake alilochangia katika kutafuta mali hizo.
2. Nadhani watoto wote (wa mke wa kwanza na wa pili) ni waislamu. Hao Islami rules will govern the administration of the deceased's properties among them.
3. Kuna issue ya illegitimate children katika Islam??? (watoto wa mkristu) Sheria ya watoto inawapa hata hao illegitimate children haki ya kurithi, subject to deceased's religious faith! sect 36(4) of child act, 2009

Wanasheria mnasemaje?
 
Yah mtoto wa kwanza ana haki kikamilifu kbsa kwasababu alizaliwa katika ndoa halali. Hapo watoto wote wana haki yule wa ndoa ya kwanza na hawa wa mama wa pili, lakini je? Mna uhakika marehemu hajaacha wosia?

Kwenye uislamu kuna rules za kugawa mali za marehemu, sio kama anavyotaka! Hivyo wosia hapa hausaidii sana! Unless anampa kama rafiki, lakini sio urithi!
 
Kama sheria haimtambui mke wa pili japokuwa kama sikosei ukishakaa na mwanamke zaidi ya miezi sita, sheria inamtambua kama mke halali, sasa iweje huyu asitambuliwe wakati amezaa na watoto.

Tuwaache wanasheria zao wapite. hapa.
 
Hapo ni miaka miwili au zaidi
 
Kwenye uislamu kuna rules za kugawa mali za marehemu, sio kama anavyotaka! Hivyo wosia hapa hausaidii sana! Unless anampa kama rafiki, lakini sio urithi!

Kwenye administration of deceased estate hakuna mtu anayeweza kuupinga wosia na kuamua kugawa mali kwa kufuata kanuni za kiimani.. Utaratibu wa kiimani unakuja pale tu panapokua hakuna wosia uliochwa na marehemu. Ingawa kwenye dini ya kiislamu wosia huzingatia mambo kadhaa kama wakfu, dhaka, thumni nk. Lakini pia mtu halazimishwi na sheria kuandika wosia kwa kufguata utratibu huu. Kumbuka kama hakuna wosia ulioachwa na marehemu aliishi kwa kufuata misingi ya dini ya kiislam hapa ndipo utaratibu wa kugawa mali kwa kutumia imani yake utatumika otherwise utafutwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa mahakama. Ndo mana nikauliza kama marehemu aliacha wosia.
 
si usubiri maamuzi ya mahakama..maana kesi si inasikilizwa huko..!!!
 
Yah mtoto wa kwanza ana haki kikamilifu kbsa kwasababu alizaliwa katika ndoa halali. Hapo watoto wote wana haki yule wa ndoa ya kwanza na hawa wa mama wa pili, lakini je? Mna uhakika marehemu hajaacha wosia?

Marehemu hakuacha wosia wa aina yoyote, kwanza kifo chake kilitokea ghafla kwa ajali ya gari.
 
hapo cjaelewa vizuri (mke mdogo anaweza kwenda kudai jasho?) anadai vipi jasho wakati aslimia 100 ya mali zilizoachwa na marehemu wamezitafuta wote pamoja, yule bi mkubwa hakufanikiwa kupata chochote chenye maana
 
Na yule mtoto wa mke wa kwanza ana haki yoyote ya kupata urithi wowote kwenye mali za marehemu ukizingatia kuwa mama yake alishapewa taraka siku nyingi hata kabla ya baba yake kupata chochote?

aliyeachwa ni mama, na ni baada ya mtoto kuzaliwa katika ndoaa iliyotambulika, mtoto ana haki zote juu ya urithi huo.
 
hapo cjaelewa vizuri (mke mdogo anaweza kwenda kudai jasho?) anadai vipi jasho wakati aslimia 100 ya mali zilizoachwa na marehemu wamezitafuta wote pamoja, yule bi mkubwa hakufanikiwa kupata chochote chenye maana

That marriage - ya muislamu-was still subsisting, ilikuwa haijavunjwa rasmi kisheria. Hivyo mkwa wa kiislamu ndiye mke halali. mama wa kikristo atadai mchango wake katika mali waliyochuma na hawala yake marehemu. Baada ya kutoa mali ya mke huyo, then likichobaki kitagawanywa kwa sheria ya kiislamu! ambayo ni dini ya mume-if he strictly confessed islam!
 
Hapana! Kuna mambo ya msingi ambayo huwezi kukuka. Kwa mfano: Katika kabila moja huko Bukoba, huwezi kukataa kumrithsha mtoto wa kwanza kama huna sabau ya MSINGI. hakuna utashi hapo. Hivyo hivyo kwenye uislamu. Sheria inasema hivyo Ukiandika wosia unaokiuka sheria hizo unakuwa batili! Ndio maana ukimrithisha mtoto wa nje ya ndoa hata kama ni matashi yako, haikubaliki.
 
Nianze na habar yako ya Bukoba ukumbuke kua Customary Laws haziwez ku over rule Statue Laws so hiyo ishu ndugu unasema haipo kabisa ndugu yangu ila isipokua tu km huyo mtu ataamua kugawa mali zake customarily.
Tuje kwenye ishu ya pili sio kwa waislam tu hata sheria imeprescribe ishu ya mtoto wa nje ya ndoa kama illegitimate child haki zake ziko limited (sijapitia The Child Act) na msaada ulioombwaa hakuna ishu ya mtoto nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…