Msaada wa kisheria plz kwa anayejua...

Msaada wa kisheria plz kwa anayejua...

Mimi sijasikia mali inagawiwa wakati Mke halali wa Marehemu (mwenye watoto watatu na ndoa hana) eti wanagawana mali walizochuma.
Navyoelewa siku hizi hata kina Mama nao wana haki ya kumiliki ardhi hivyo kikwetu /Kabila yetu huwezi gawa mali wakati mama bao yupo hai eti Mwanamume katangulia.
Ngoja tuangakie hizo Sheria nyingine za Ndoa na Dini wanaemaje wachangiaji
 
Jamaa alioa mke na kufunga nae ndoa (ya imani ya kiislam) japo haikudumu sana ingawa walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume na wakapeana taraka kila mtu akaendelea na maisha yake huku mwanamke akipata bwana mwngne na mme kuchukua mke (mkristo) mwngne na kuendeleza nae maisha na kufanikiwa kupata watoto watatu japo hawakuwahi kufunga ndoa ingawa wameishi pamoja kwa miaka 13 sasa.
Kwa maisha aliyoishi na huyu wa pili walifanikiwa kununua kiwanja na kujenga nyumba japo ujenzi wake haujakamilika.
Bahati mbaya jamaa ameisha fariki (kama miezi mitano imepita tangu afariki), hivi sasa kumeibuka mgogoro wa kifamilia kati ya wake zake wote japo yule wa kwanza walishapeana taraka na huyu wa pili hawakufanikiwa kufunga ndoa kwa miaka hiyo yote walioishi pamoja.
Sasa yule mke mkubwa kaenda mahakamani kudai mali alizoziacha mtaraka wake kuwa mwanae ndo mwenye haki na mali zile zote kwani hawa watoto hawana haki ya kumiliki chochote kwa 7bu baba yao hakuwahi kufunga ndoa na mama yao.
Kwa sasa kesi ipo mahakamani na mahakama imezuia uendelezaji wa aina yoyote kwny jengo/nyumba aliyoicha marehemu.

Je, kisheria nani mwenye haki wa umiliki wa mali za marehemu?
mke wa pili ana haki zote kwani walichuma mapema, mke wa kwanza hana haki na mali izo ila mtoto anapaswa kupata mgao wake kama mrithi halali wa baba yake kwani alipatikana katika ndoa.
 
Back
Top Bottom