msaada wa kisheria plzzz........!!!!!

veshego

Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
17
Reaction score
20
habarini wanajamii.... naombeni msaada wenu wa kisheria katika jambo hili linalohusu familia yetu!

sisi tumezaliwa watoto sita katika familia yetu na kila mmoja na mama yake!baba yetu alikua anaish na mama yangu lakini walitangana na baba akamchukua mama mwingine wakawa wanaishi wote. baada ya miaka kadhaa baba alifariki na sis tulikuwa wadogo bado tunasoma sekondari! hivyo ikatokea kumchagua mama yetu wa kambo kuwa msimamizi wa mirathi baada ya ugomvi mkubwa kati mama yetu wa kambo na bamdogo zetu!tatizo tulilokuwa nalo saiv ni kwamba huyu mama kapangisha nyumba nzima halaf kahamia kwao manyara anakuja kuchukua kodi kila baada ya miezi sita na sisi hajatuaga! pia nyumba yetu imeharibika vibaya mno na inataka kudondoka! hivyo sis kama watoto tunajipaga tukamtengue huyu mama kama msimamizi wa mirathi tunataka tusimamie wenyewe kwan nyumba imemshina kusimamia na ameuza baadhi ya mali bila kutushirikisha!
je kisheria tutafanikiwa kumtengua huyu mama usimamizi wa mirathi? ni vitu gan vitahitajika? naombeni ushauri wenu wadau!
 

Inawezekana sana tena sana. Kuna mambo ya kisheria ambayo lazima umuone mwanasheria akuelekeze. Hapa itakuwa vigumu kuyajadili.
 
Inawezekana sana tena sana. Kuna mambo ya kisheria ambayo lazima umuone mwanasheria akuelekeze. Hapa itakuwa vigumu kuyajadili.


Watafungua shauri kama watoto au kupitia kwa mama yao?

Kwa sababu kasema kuwa Baba na mama yao walitengana (separate) na hakuwa wameachana (divorce)!
 
Watafungua shauri kama watoto au kupitia kwa mama yao?

Kwa sababu kasema kuwa Baba na mama yao walitengana (separate) na hakuwa wameachana (divorce)!
Kama wao as long as they are not minors! Sijui umri wao, Kama ni wakubwa, wao kama beneficiaries wanapinga msimamizi wa mirathi kwa kutawanya mali zao, sheria iko wazi. Ni waislamu, wakristo , wa nje ya ndoa, time limitation etc ndio maana nasema wamuone wakili
 
Nendeni kwenye vitu vinavyotoa misaada ya sheria. Kuna wlac sema kinatoa kwa wanawake kama mnadada aende kuwaona hichi kipo kinondoni, kuna tanganyika law society office zao zipo mikocheni, kuna school of law kipo chuo kikuu cha dsm alizia kutovi cha sheria kipo wapi.
Maelezo uliotoa hatajitoshelezi, na kesi za mirathi zina mambo mengi. Nivizuri uonane na wakili akusaidie.
 
Mara nyingi watu wanaoteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi huwa wanajisahau na kufikia hatua ya kudhani kuwa jukumu walilokabidhiwa ni kumiliki mali badala ya kuzisimamia.Msimamizi wa mirathi anayo majukumu matatu ya msingi;Kukusanya mali za marehemu,kulipa madeni,kugawanya mali na mwisho katika kipindi kisichozidi miezi sita kuwasilisha kwenye mahakama iliyomteua mchanganuo(inventory)wa mali na jinsi zilivyogawanywa.Kwa kuwa suala lilikuwa ni kumwamini,lakini muhusika ametenda kinyume na majukumu yaliyoko hapo juu,basi nyinyi kama wafaidika(beneficiaries),au warithi,mnayo haki ya kuhoji mwenendo huo mahakamani,kwa kupeleka pingamizi kwa ushahidi wenye kujitosheleza.Ikidhibitika,mahakama yaweza kutengua usimamizi,na kumteua mtu mwingine badala ya huyo wa Mwanzo.
 
inawezekana tena kwa urahisi sana, ila hii siyo ishu ya kujadili hapa jf namna hii, uko mkoa gn? from advocate Makundi
 
Una umri gani? kama kuna aliyezidi 18, na mnamuamini, mnaweza kubadilidha msimamiz wa mirath kwa kua na ushahid na mashahidi kuonyesha kua huyo mliye nae hafai
 
Inawezekana kumtengua, mnapaswa kuandaa sababu za kutosha kuonyesha ameshindwa kazi yake. Pia hakuteuliwa kuwa mridhi bali msimamizi, usimamizi una mwisho, nyie mmeahakua wakubwa
 

mbona tatizo dogo sana hili bwana ndugu ingawa swali lako limekaa Ki-assignment hv kwanza tafuta pdf hizi kwenye google probate and administration of estate Act(ya tanzania) naamini kuna section zinaendana na issue yako(nilisomaga zamani sana)
 


Vieshego:

Kwanza pole na yote yanayowasibu wewe pamoja na ndugu zako.

Awali ya yote, naomba utujuze maswali yafuatayo kabla hatujatoa ushauri:

Mosi: Je, ni kikao gani kilikaa na kumteua mama yenu (wa kufikia) kuwa msimamizi wa mirathi? Mara nyingi kikao cha wanafamilia /wanaukoo ukaa na kufikia maamuzi haya;

Pili, Je mama yenu alifungua mirathi katika mahakama yoyote kuomba kuteuliwa kama msimamizi wa mirathi?

Je, marehemu baba yenu aliacha wosia? alikuwa ameoa kwa mujibu wa sheria za nchi?

Tatu: wakati baba yenu anapatwa na umauti alikuwa anaishi kindoa na huyo mama?

Nne, Je baba yenu ni muumini wa dini gani? au mpagani? na alikuwa ameoa na kuwataliki mama zenu (waliowazaa) au alikuwa amewazalisha tu?

Wasalaam,

Shadow.
 
ahsanteni wadau kwa ushauri wenu..!!!
Shadow majibu ya maswali yako ni kama yafuatayo
1.kikao kilichokaa ni cha majirani na viongoz wa mtaa.... kwa upande wa ndugu alikuwepo baba yetu mdogo peke yake na watoto wawili kati yetu sita kwani wengine tulikuwa tumesharud shule pamoja na majirani

2. ndio mama yetu aliiandikia barua mahakama ya mwanzo kuomba kuwa msimamiz wa mirathi baada ya kikao cha ukoo kilichofanyika tanga na kumchagua bamdogo kuwa msimazi wa mirathi kwani sis hatuish tanga tunaish mbeya na mzazi wetu alizikwa huko hvyo baada ya kuzika tulirud mbeya siku hiyohyo na ndugu wa baba walibak tanga na baada ya tatu walimchagua bamdogo kuwa msimamizi!
3. baba yetu hajawahi funga ndoa na mama yyte yule na hajawah kuacha wosia. pia mauti ilimkta akiwa na mama yetu wa kambo. pia baba yetu ni musilamu.
 
mkuu, maswala ya mirathi yanamikanganyiko mingi. Upo uwezekano wa kutengua usmamiz endapo tu "KUTAKUWA NA SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA HIVYO." kutokana na kwamba mambo haya yanamaswala mengi ya kujua na maelezo yako yamekosa vingi vya msingi na hata hvo ni vyema mtu akapata wasaa wa kupitia baadhi ya nyaraka hvo ni ngumu mtu kukushauri vyema. Hapa unaweza ulizwa hata maswali ambayo kwa wakati huu hata siyo ya msingi. Kama unaweza kulipa bill ya wakili wa kujitegemea ni vyema ukamuona kama huwezi fata ushauri wa taxbabe
 
Last edited by a moderator:
u have a point, ila ni kama cardiovascular surgeon atoe maelezo hapa ili mtu ambaye siyo daktari atumie kwa ajili ya kumfanyia mgonjwa upasuaji
 
zamani sana muda gn? probate and administration of estates Act ni procedural, zaidi ni Magistrates courts Act, na kuna sheria ambazo ni substantive kutokana na imani ya mtu ie mkristu, muislam na mpagani, na pale ambapo kuna wosia hizi sheria msingi zina utaratibu wa ni nini kifanyike pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…