Msaada wa kisheria tafadhali

mutagaywa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
891
Reaction score
189
Wakuu,

Kama nilivyotaja kuna bwana mmoja nilikuwa nafanya nae kazi lakini kutokana na kutokuwa mwaminifu nimevumilia siku nyingi kuusu utendaji wake wa kazi na hisitoshe alikuwa mtu wangu wa karibu sana lakini baada ya kuonekana kutokuwa mwaminifu katika kazi ambayo tulikuwa tunashirikiana niliamua kuvunja makubaliano yangu nae nakuamuru anilipe staiki zangu ili yeye aendee kufanya kazi hiyo lakini alishindwa kufanya hivi.

Ndipo nilipoamua kumpeleka baraza la kata kupata muafaka lakini cha kushanza baraza la kata linakuja na huku nyepesi yakuniambia eti mimi nimeshidwa hivyo huyo bwana itanibidi anipe hela kidogo ambayo aifiki hata robo nimekataa wakasema kama nakata rufaa kwenda mbele inabidi nilipe elfu kumi kwa ajili ya wajumbe nimelipa hiyo pesa, natarajia kukataa rufaa kupinga hukumu hiyo uchwara sasa.

Naomba msaada wenu kuhusu hiyo rufaa coz ndo mara yangu ya kwanza kudhuru mahakamani tafadhali kitu gani inabidi nifate.

Asanten sana.
 
Mkuu ungetoa maelezo ya kutosha, hiyo kazi mliyokua mnafanya ni halali? makubaliano yenu yalikua na maandishi? kama ndio kwenye hayo maandishi mliweka terms zozote za namna ya kuvunja makubaliano? je hicho kiasi unachodai unaweza kukithibisha mahakamani bila shaka kuwa ndicho kiasi halali unachopaswa kulipwa? wakati unavunja makubaliano yenu mliachana kwa utaratibu upi? umiliki wa hiyo kazi / biashara ulikua unashare kwa mtindo upi?
 
Na pia kama unao ushahidi wa yeye kuvunja uwaminifu?? Si kwa maneno tu.
 
Ushahidi hupo sema kuvunja mkataba hapo naona kama ndo nilibugi but vielelezo vyote niliambatanisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…