Habari wakuu,
Hivi ikitokea mti uliopo kwenye eneo lako(kwa maana ya ardhi) ukaangukia upande wa jirani mnae pakana nae na ukaleta madhara yawe makubwa kama kuua au madogo mfano kulalia bati likapinda au kuvunja sehem ya choo nk bila mti huo kusababishwa na mtu km kukatwa,ni kwamba umeanguka wenyewe tu au sehemu ya tawi limekatika labda kwa upepo,je mimi mmiliki wa mti huo(eneo) nitakua na kosa kisheria?,
Tusaidiane uelewa.
Ahsante.
Hapana hautakua na kosa, kama utakua umeangushwa na upepo
Kuna defence (utetezi kisheria) unaweza kuutumia, unaitwa ACT OF GOD (Yaani matendo ya mungu). Huu utetezi hua unatumika pindi jambo linapotokea ambalo halipo katika uwezo wa mwanaadamu (either kuliona au kulizuia) na kuleta athari fulani.
Mfano gari yako imechukuliwa na mafuriko, wakati wewe upo ndani ya gari unaendesha, na kwenda kugonga nyumba ya mtu, na kuzua hasara. Huwezi kushitakiwa kwa kosa la kuharibu mali ya mtu kwasababu jambo lililotokea ni nje ya uwezo wako (huwezi kuzuia mafuriko).
Mfano wa utetezi wa Act Of God,
1) Mvua kubwa au mafuriko.
2) Upepo Mkali.
3) Radi.
4) Tetemeko la ardhi.
5) Mlipuko wa moto pori.
6) Mmomonyoko wa Mlima. N.k
NB Sheria inakulazimu kua mwangalifu na kutoku sababisha madhara kizembe kwa mwenzako, na kuwa makini kwa vitu unavyomiliki vinavyo weza kuleta madhara kwa mwingine. (Ukifuga mbwa mkali, ni wajibu wako kuhakikisha unaweka onyo nje ya uzio wako, na kumdhibiti asije kumdhuru mtu yoyote. Pindi atakapo toroka usiku bila wewe kujua, basi utakutwa na hatia ya uzembe STRICT LIABILITY)
I stand to be corrected,