kissa anyigulile
JF-Expert Member
- Apr 21, 2017
- 1,550
- 1,742
Nilikuwa na rafiki yangu, alikuwa ameajiriwa katika shirika moja zuri tu, katika position nzuri tu.
Siku moja alimfumania mke wake na jamaa fulani chumbani kwake wamekaa kitandani wakiangalia ponografia.
Paap! Mke akachoropoka, wakabaki wawili chumbani, mfumania na mfumaniwa.
Ngumi zikaanza, tap tap, tap tap!
Mfumaniwa akapigwa moja makini sana, akadondoka chini tuup! Ili kumaliza kazi, mfumania akaongezea na tofali la kichwa paap!
Mfumaniwa akapoteza maisha palepale!
Kesi ikaenda Polisi, mahakamani. Mfumania alikaa ndani kama miaka minne hivi!
Jamhuri ilitafakari ikaona kwa kweli mfumania hakutendewa haki kabisa, hivyo ikamwachia huru!
Sasa uchungu wangu ni kwamba Jamaa alivyorudi kazini akawa amepoteza kazi!
Swali langu: Kama Jamhuri ilimuonea huruma na kuona kwamba jamaa hakutendewa haki, kwa nini isiwe hivyo na kwa mwajiri pia?