mbung'o muba
Member
- Apr 2, 2012
- 10
- 1
aisee facts hazijakamilika kabisa, umekamatwa wapi eneo gan lilipokuwepo hilo gari?hilo gari lilikuwa linafanya nini na ni daladala au gari binafsi? umekamatwa na nani?je ulitwa kwenye kikao kilichotoa hayo maamuzi?je umepewa barua ya kufukuzwa kwako? maswali mengine yatafuataNimesimamisha masomo ya chuo kikuu kwa kukamatwa na wenzangu tukiwa kwenye gari ambalo ndani yake kulikuwa na wenzetu wamevaa nguo na nembo za CHADEMA nakuambiwa wote ni wafuasi wa chama na kutupelekea adhabuhiyo toka chuo kikuu Dodoma (UDOM). Nahitaji kwenda Mahakamani, Je! nianzie wapi mimi si mtaaramu wa sheria na sijawahi kuingia mahakamani?
sasa kabla hujaenda mahakamani angalia kwenye prospectus yenu ya chuo inatoa remedy gan kwa mtu ambaye amefukuzwa chuo lakini hajaridhika na maamuzi yaliyotolewa, mfano, anaweza kukata rufaa wapi?ikiwa kimya then hapo ndipo unaweza kuomba mahakama iquash decision ya UDOM dhidi yakoNilikuwa katika safari zangu,kwenye daladala toka chuo kuelekea mjini ndipo gari ikazuiliwa getini na kuamriwa irudi chuoni kwamba amri imetolewa na uongozi wa chuo gari hilo lizuiliwe. Kufika utawala akatokea moja ya viongozi wakuu wa chuo na viongozi wandamizi , waka hoji kuna wanakijiji ndani kwenye gari watu wakajibu ndio, wakaambiwa washuke, wakashuka watu kama 10. kisha ikatolewa amri kuwa wanafunzi wote wahakikishe wanavitambulisho, ndipo wanakijiji wakaamriwa kuendelea na safari nawanafunzi kushikiliwa.swli lililo ulizwa na mkuu huyo ni kwa nn mnajihusisha na siasa?wakanyang'anya vitambulisho na kutuambia tusubili barua zetu. Hakuna aliye hojiwa mkuu, na hii ilitokana na kuwa kwenye kari hilo kulikuwa na wanafunzi 5 wakiwa na nguo nembo za chama.hivi ninapo ongea barua hiyo nipo nayo na nipo nyumbani.