Mkuu Kidume, pole kwa kupitwa na wakati.
Zamani wakati ukijiunga ni kweli unajaza mahali pa kuchukulia mafao yako kwa sababu wakati huo mafao yalikuwa yakilipwa kwa malipo ya hundi.
Sasa mafao hayalipwi kwa hundi bali unaingiziwa kwenye account yako popote ulipo. Huna haja ya kwenda popote kuchukua mafao yako zaidi ya ndani ya account yako.
Mifuko yote mitano ya hifadhi ya jamii inazo ofisi zake kila mkoa. Hivyo 6 months kabla ya tarehe yako ya kustaafu, mwajiri anakujulisha kwa barua kuwa umebakiza miezi 6 kustaafu ili ujipange. Copy ya barua hiyo pia inakwenda kwenye mfuko wako.
One moth kabla hujastaafu unapewa barua na likizo ya kustaafu ukirudi kazini ni kuchukua tuu barua na kuiwasilisha kwenye mfuko as a procedure tuu lakini mifuko mingine, mafao yako yanakuwa yameishaingia kwenye account yako hata kabla hujastaafu.
Ukisha staafu unachotakiwa kufanya nI kutoa tuu taarifa ya mahali ulipo settle kwa ajili ya zoezi la uhakiki.
Unataka kufungua kesi kwa lipi? . Mafao yako ni haki yako na uko huru kuyapokelea popote unapotaka wewe, kupitia benki yoyote.
Pasco