Kubadili umiliki wa gari TRA sasa hivi wanahitaji vifuatavyo:
1.Kadi halisi ya gari husika
2.Mkataba wa mauziano kutoka kwa mwanasheria, ukiainisha maelezo muhimu na ukiwa umesainiwa na wahusika pia muhuri wa mwanasheria
3.Stakabadhi(risiti) ya mwanasheria kuonesha kwamba mkataba huo umelipiwa(Inatakiwa risiti ya EFD)
4.Kitambulisho na picha (passport size) ya muuzaji
5.Kitambulisho na picha ya mnunuzi
Haya ndio niliyokutana nayo mie wiki ilyopita nadhani bado mengine yaweza ongezeka
PIA nilipeleka kadi kubadili rangi na engine namba nimetakiwa kuambatanisha VIR(Vehicle Inspection Report), EFD risiti ya garage iliyofanya matengenezo
Kwa kifupi mambo ni mengi na unahitaji kuwa na muda