MSAADA WA KISHERIA. Unapotaka kununua Gari kwa mtu

edward pais

Member
Joined
Aug 16, 2016
Posts
38
Reaction score
60
Wanajamvi naomba kujuzwa ni utaratibu upi wa kisheria mnunuzi wa gari unaufata unaponunua gari kwa mtu. Mfano ni nyaraka zipi unatakiwa upewe na mwenye gari au nyaraka zip unapeleka TRA kibadili jina la mmiliki. Kwa
 
Kubadili umiliki wa gari TRA sasa hivi wanahitaji vifuatavyo:
1.Kadi halisi ya gari husika
2.Mkataba wa mauziano kutoka kwa mwanasheria, ukiainisha maelezo muhimu na ukiwa umesainiwa na wahusika pia muhuri wa mwanasheria
3.Stakabadhi(risiti) ya mwanasheria kuonesha kwamba mkataba huo umelipiwa(Inatakiwa risiti ya EFD)
4.Kitambulisho na picha (passport size) ya muuzaji
5.Kitambulisho na picha ya mnunuzi

Haya ndio niliyokutana nayo mie wiki ilyopita nadhani bado mengine yaweza ongezeka

PIA nilipeleka kadi kubadili rangi na engine namba nimetakiwa kuambatanisha VIR(Vehicle Inspection Report), EFD risiti ya garage iliyofanya matengenezo

Kwa kifupi mambo ni mengi na unahitaji kuwa na muda
 

Umesahau nakala ya TIN
 
na Copy ya Tin ya Mnunuzi.

Pamoja na malipo: (Stamp Duty 1% (bei mauziano ya gari), Transfer of ownership - 50,000/= na hela ya ku print kadi mpya - 10,000/=).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…