Msaada wa Kisheria: Warithi wa kike wanadhulumiwa haki zao za msingi na mtoto wa Nje ya Ndoa

Msaada wa Kisheria: Warithi wa kike wanadhulumiwa haki zao za msingi na mtoto wa Nje ya Ndoa

Kweli usemalo mda sio mrefu nmeambiwa wameenda kwa M/kiti wa Mtaa tatizo huyo kijana asikii la muadhini wala mteka maji msikitini anaweza akaenda kuwenywea pombe na kuwavutia bangi kisha akaja kuwatukana wamama wawatu
Ikiwa atafanya hivyo achukuliwe hatua za kinidhamu...ashitakiwe kwa kosa la kutukana na matumizi ya dawa za kulevya! Poleni sana binadamu tumeumbwa tofauti tofauti na madhaifu ili kusaidiana!
 
Ikiwa atafanya hivyo achukuliwe hatua za kinidhamu...ashitakiwe kwa kosa la kutukana na matumizi ya dawa za kulevya! Poleni sana binadamu tumeumbwa tofauti tofauti na madhaifu ili kusaidiana!
Yaani mtu huyu ukiambiwa mambo anayoyafanya huwezi kuamini mpaka hawa wa mama wanamuogopa alafu kitu kingine jamaa ni mtu wa kalumanzila balaa! Hivyo ndo maana hawa wa mama wanataka suluu na yeye sema yy ndo kichwa mchunga haelewi chochote wala kusikia
 
Ni msukuma?
 
Ndugu wanajamvi kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba tuungane kusoma yanayowasibu ndugu zetu

Kuna familia moja ambayo mpaka sasa ina watoto 6 wengine wameshatangulia mbele za haki ambao wamezaliwa na baba mmoja lakin wanne kati yao wamezaliwa na Baba mmoja na Mama mmoja,

alafu mtoto mwingine kazaliwa na Baba mmoja pamoja na wale wanne lakini kwa mke mwingine ,
Alafu wa mwisho ni mtoto wa kiume ambaye kazaliwa nje ya ndoa huyo ndio sababu ya kuandika Uzi huu

Kimsingi huyu mtoto wa mwisho 6 ambaye kazaliwa nche ya ndoa amekuwa Msumbufu, Mgomvi na akiwaonea watoto halali wa familia ya Mzee Saidi kisa eti ni watoto wa kike.

Ndugu hawa wameachiwa Nyumba moja kubwa na ina uwanja mkubwa lakin kwa sababu wao wamekuwa ni watoto wa kike basi huyo mdogo wao wa njee ya ndoa amekuwa akiwapelekesha anavyotaka yeye.

Imefikia stage wamepangisha mpangaji katoa hela ya pango kisha wakagawana pamoja na huyo mtoto wa njee ya ndoa lakin yeye ameamua kumleta mpangaji mwingine nakumpangisha bila ya kuwa shirikisha wenzie jambo ambalo limeleta mgogoro mkubwa kiasi kwamba mpangaji wa mwanzo anataka arudishiwe kodi aliyoitoa.

Sasa hawa ndugu wa 5 kodi wamesha gawana na wameila, alafu sasa hivi mpangaji wa awali amekuja juu anataka pesa zake arejeshewe kwaiyo kumetokea mgogoro mkubwa mpaka sasa haujatatulika

Ndugu hawa 5 wameona sasa bora wauze nyumba yao hiyo ili wagawane hela mambo yaishe lakin cha ajabu huyu mtoto wa nje ya ndoa hataki nyumba hiyo iuzwe anataka aendelee kuitawala atakavyo kisa warithi hao ni watoto wa kike ya yeye ni mwanaume

Je ndugu wanajamvi hawa watoto halali wa mzee said ambao wapo 5 wafanye nini iliwapate haki yao

Nawasilisha....!!!!
Wakafungue mirathi kwa sheria za kiislamu hapo watakuwa wameweza kum outsmart mtoto wa nje ya ndoa..
 
Sharia ya mirathi kwa dini ya kiislamu haimtambui mtoto wa nje... Huyu anaitwa mtoto wa haramu.
Ndo maana anawasumbua
 
Thubutu asije wakati tunalima mihogo akajumuika atusumbue kisa nini?? Hatumpi attention ahangaike na maneno yake kila mtu apewe chake na mahakama tusijuane,. Japo siko level ya kutafuta mali za urithi zangu zinatosha.
 
Yaan huyu mtu kashindwa kujitafutia maisha kaamua kuja kuwa kaba wa mama wawatu
 
Waache ujinga hao.....(sorry kwa lugha kali)

Hilo ndilo tatizo.kubwa.

Wajitambue wajue haki zao kwanza
 
Mungu wangu..huyo mtoto kwa vile ndio haramu ndio maana..pole sana
 
Yaan huyu mtu kashindwa kujitafutia maisha kaamua kuja kuwa kaba wa mama wawatu
Kwetu mwanamke haruhusiwi kurithi mali za baba yake, hao kina waache kutolea macho hizo kama wameolewa watulie wale mali za waume zao.
 
Waswahiliwalisema, mtegemea cha ndugu,hufa masikini.

Pia walisema, cha mtu mavi.

Binafsi sitaka kushobokea mali ya urithi.
 
Wasikubali kuuza nyumba kwa ajili ya juha huyo.Watoto wote ni sawa bila kujali jinsia.Wampeleke mahakamani asiwasumbue hana lolote ila waanze kwa mwenyekiti wa mtaa ama kijiji.
 
Back
Top Bottom