Kifungu na.38 cha Sheria ya kazi na mahusiano kazini 2004 inasema kwamba iwapo mwajiri anataka kufanya redundancy afanye yafuatayo:-
(a) kutoa notice ya nia ya kupunguza wafanyakazi;
(b) kuweka wazi information zote muhimu za jinsi ya kupunguza wafanyakazi na nia ya kufanya hivyo kwa ajili ya kupata mawazo kwa wafanyakazi;
(c) kutafuta maoni ya wafanyakazi kwa ajili ya yafuatayo-
(i) sababu za kufanya punguzo hilo;
(ii) njia zilizo na zitakazosaidia kutokupunguza wafanyakazi;
(iii) vigezo vitakavyotumika kuchagua wafanyakazi watakaopunguzwa;
(iv) muda zoezi litakapofanyika; na
(v) malipo kwa watakaopunguzwa,
(d) kutoa notice, kuweka wazi info za zoezi la kupuguza wafanyakazi, kwa-
(i) vyama vya wafanyakazi vinavyotambuliwa na kifungu na 67;
(ii) kwa vyama vya wafanyakazi vya ndani vilivyosajiliwa;
(iii) mwakilishi yeyote wa mwajiri na kwa ambaye hana mwakilishi basi kwa mtu yeyote anayetambulika naye au chama.
(2) Pale ambapo consultations zimefanyika na hakuna makubaliano kati ya mwajiri, waajiriwa na vyama vya wafanyakazi juu ya jinsi ya kupunguza wafanyakazi, basi suluhu yaweza patikana kwenye Tume ya Uamuzi na Usuluhishi (CMA).
(3) Pale ambapo, mfanyakazi amepunguzwa kazi kwasababu amekataa kukubali mabadiliko ya ajira, mwajiri anawajibika kudhibitishia mahakama ya kazi kwamba isingewezekana kampuni kuendeshwa bila mabadiliko hayo.