Habari za wakati huu wakuu humu ndani ,jamani mimi naomba kuuliza kwa wanaojua sheria za uhamiaji ,nina rafiki mmoja tulifahamiana sehem ya kazi yeye ni MCHINA sasa nimepata taarifa kuwa alikamatwa na watu wa uhamiaji wamemuweka ndani kwa zaidi ya mwezi sasa ?swali langu ni je kama labda kuna mambo alikiuka je ni sahihi kumshikilia kwa siku zote hizo ,na je nini haki zake hata kama alikosea?? Asanteni.