Msaada wa Kisheria

Sidhani kama hiyo BUKTA ina-bear definition ya "UNIFORM".

KWA MUJIBU WA KANUNI ZA ADHABU, SURA YA 16, KAMA ILIVYOFANYIWA MAREJEO MWAKA 2002, KIFUNGU NAMBA 178; ni uhalifu kuvaa Uniform ya Jeshi / Polisi kama wewe si askari au mwanajeshi wa majeshi mbalimbali yaliyopo nchini. (jeshi la polisi, jeshi la magereza, Jeshi la JWTZ nk).

Sio tu kuvaa Uniform hiyo, bali pia kuvaa uniform inayofanana fanana, au yenye kutaka kufanana fanana hivi na uniform husika.

Vilevile ni Uhalifu kuvaa mavazi ya jeshi/ Polisi, au mavazi yanayofanana na uniform za jeshi/Polisi, KWA MALENGO YA KUDHIHAKI MAVAZI HAYO.

Adhabu yake ni kifungo CHA MWEZI MMOJA JELA.

LAKINI MTU ATARUHUSIWA KUVAA UNIFORM HIZO ENDAPO ANAFANYA MAIGIZO YA JUKWAA, AU KAMA ANAFANYA STAGE SHOWS ZA MUZIKI, AU KAMA ANAFANYA MAONESHO YA GWARIDE LA JESHI.

Cc Malcom Lumumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…