TOPLINE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 418
- 489
Samahani kwa usumbufu pia wakubwa zangu shikamoo mimi ni kijana niko chuo mwaka wa tano xaxa hivi baba yetu alifariki mwaka 1998, na alituacha mawili tu na mdogo wangu ambaye naye yuko chuo shida ninayoipata ni kwamba msimamizi wa mirathi hatujali hata kwa kile kidogo tangu mwaka 1998, xaxa hivi nadaiwa ada imefikia hatua mama,anashidwa kutulipia ada kutoka na madeni mengi,na huyu msimamizi wa mirathi tukiomba msaada tunaambulia vitisho tu, isitoshe ameuza nyumba aliyoiacha baba pia amefunga hisa zote alizokuwa nazo mzee kila tunapooomba msaada ni vitisho na ahadi zisizo timia, mama amesumbuka toka nikiwa darasa la kwanza mpaka leo watu wapo tu wamekumbatia miradhi isiyo yao, imefikia hatua tunashidwa kuendelea na chuo kwasababu ya madeni jamaani naombeni mtu yeyote anisaidia tupate miradhi yetu au anipe mwongozo , mahakamani mambo ni magumu hawa watu wanapesa na wanatutambia na kutuambia hata mkienda mahakamani hampati kitu nisaidie hata kama kuna chama kinachotoa msaada tupate mirathi yetu niweze kwenda, naombeni msaada