MSAADA WA KISHERIA

MSAADA WA KISHERIA

TOPLINE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
418
Reaction score
489
Samahani kwa usumbufu pia wakubwa zangu shikamoo mimi ni kijana niko chuo mwaka wa tano xaxa hivi baba yetu alifariki mwaka 1998, na alituacha mawili tu na mdogo wangu ambaye naye yuko chuo shida ninayoipata ni kwamba msimamizi wa mirathi hatujali hata kwa kile kidogo tangu mwaka 1998, xaxa hivi nadaiwa ada imefikia hatua mama,anashidwa kutulipia ada kutoka na madeni mengi,na huyu msimamizi wa mirathi tukiomba msaada tunaambulia vitisho tu, isitoshe ameuza nyumba aliyoiacha baba pia amefunga hisa zote alizokuwa nazo mzee kila tunapooomba msaada ni vitisho na ahadi zisizo timia, mama amesumbuka toka nikiwa darasa la kwanza mpaka leo watu wapo tu wamekumbatia miradhi isiyo yao, imefikia hatua tunashidwa kuendelea na chuo kwasababu ya madeni jamaani naombeni mtu yeyote anisaidia tupate miradhi yetu au anipe mwongozo , mahakamani mambo ni magumu hawa watu wanapesa na wanatutambia na kutuambia hata mkienda mahakamani hampati kitu nisaidie hata kama kuna chama kinachotoa msaada tupate mirathi yetu niweze kwenda, naombeni msaada
 
MY FRIEND TAFUTA WAKILI MUELEZE HIYO CIRCUMSTANCES... MWANZO MLIKUWA WATOTO...SASA HIVI MMEKUWA...KOMAA AKILI ACHA UTOTO...
 
Wakili E.Mselewa anga zako hizi...toa msaada
 
Duh!
Hapo ndugu yangu ni kumwomba Mwenye Enzi Mungu aingilie kati, maana wakili atatafuna hivyo vijipesa vyenu vilivyo baki na likesi lika nguruma mahakamani hata miaka kumi walahi
Kuna kitu kikubwa cha kujifunza hapo jamani
Kina baba muwe mna wa julisha wake zenu mali mlizo nazo jamani!
Nakushauri usihangaike kabisa na mahakama mdogo wangu!
 
Kuna sheria za mirathi zinazotumika Tanzania ziko tatu
1. Sheria ya kimila
2. Sheria ya kiislam
3. Sheria ya kiserikari iitwayo "Indian succession act"
.
Kuna wajibu wa msimamizi wa mirathi.
1. Kukusanya mali za marehemu, hii ni pamoja na madeni aliyokuwa akidai.
2.Kulipa madeni halali aliyokuwa anadaiwa marehemu.
3. Kugawa mirathi kwa warithi halali.
4. Kutengeneza taarifa juu ya ukusanyaji na ugawaji wa mali za marehemu na kuwasilisha taarifa hiyo mahakamani ndani ya miezi sita toka alipopewa usimamizi.
.
Msimamizi asitetimiza wajibu wake.
Msimamizi anayefuja mali za marehemu au asiyetimiza wajibu wake anaweza kuchukuliwa hatua zakisheria.
.
Mahakama inaweza kuombwa kumnyang'anya usimamizi na kisha msimamizi huyo kuamriwa kulipa au kurejesh mali alizotumia vibaya au kufuja.
.
MUHIMU:
Mjane anapaswa kushiriki na kutoa mchango wake katika kikao cha wana ukoo kumpendekeza msimamizi wa mirathi ya marehemu.
2. Mjane ana haki ya kuomba usimamizi wa mirathi ya marehemu mume wake.
3. Msimamizi wa mirathi hatakiwi kunufaika kwa hali yoyote ile na mali za marehemu isipokuwa kama yeye ni mmoja wa warithi halali.
.

Mzee hilo sisi tunaita dili unapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom