MSAADA WA KISHERIA

Wilhelm Johnny

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2016
Posts
1,368
Reaction score
1,325
Habari za asubuhi wakuu niilikua naomba msaada wa kisheria juu ya uharibifu wa mazao nasema uharibifu wa mazao kwa sababu kama mtu kakuharibia kifaa cha shamba kwa makusudi na kusababisha mazao kukauka si sawa na kuingia shamba kuharibu mazao. na huyu kijana hii nitabia yake kufanya vurugu na kuharibu vitu akipelekwa polisi mama yake hutoa hongo na kesi zinapindishwa. Huyu kijana amekatakata mpira wa mita 50 niliokua natumia kunyeshelea kwenye mboga na mipapai. Mimi nina RB yake hapa wiki ya pili nikipiga mahesabu ya kwenda Polisi nikifikiria na fedha watakazohitaji na hapa sina chochote naishia kukata tamaa kama kuna aliyeko moshi na anauwezo wa kunisaidia jamani naomba msaada wake kisheria huyu kijana aadhibiwe kwa kosa alilofanya maana mtu najitahidi kupambana siibi cha mtu ni jitihada zangu mwenyewe bado kuna kuja mtu anafikiria kukurudisha nyuma. Naambatanisha na picha za eneo la bustani lililoharibiwa na ukame baada ya mpira kukatwa katwa. Nina Ishi Moshi Mjini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kijana sio chizi kwamba aanze tu kuja kukata mpira..umemkosea nini?
Una ushahidi kwamba yeye ndio aliyekuja kukata hapo?
 
Huyo kijana sio chizi kwamba aanze tu kuja kukata mpira..umemkosea nini?
Una ushahidi kwamba yeye ndio aliyekuja kukata hapo?
mkuu kisa ni cha kipumbavu kabisa na hakilingani na mpira aliokata nikikuhadithia utajua tu kijana alikua na wivu na wakati anakata nilikua namuona na ndugu kadhaa hapa nje. na RB yake nimekata tatizo ni kuwa polisi ukifika tu kuja kukamata muhalifu unatoa 20000 ya mafuta hapo bado hujazungushwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kijana sio chizi kwamba aanze tu kuja kukata mpira..umemkosea nini?
Una ushahidi kwamba yeye ndio aliyekuja kukata hapo?
Ilikua hiv huyu kijana ni mtoto wa mama mdogo anatabia ya kufanya vurugu nje hapa na ni mwaribifu mkubwa sana ila mama yake humkingia kifua kwa kuhonga maaskari. Majuzi alinituma simu yake iko chaji kwa lengo la kuuza akiahidi kunipa 1000 kama ujira wa kunituma. Na kweli alifanikiwa kuuza nikamuomba aniazime 1000 iwe 2000 akatii na kunipatia siku ananidai nikamrejeshea 1000 akakataa akidai anataka 2000 yote hapo ni akiwa kalewa nikamwambia sawa kwa kuwa sasa sina hiyo cash maana nilikua home subir mother arejee nikupe. Na kwa kuwa tayari alikua ameshashikilia mpira wangu wenye thamani ya 60000 elfu. Nikamwambia mpra si unao kiongozi nitakupa jioni. Akaanza ooh kwani mpira unanini naweza uweka bondi mara au niukatekate saivi ghafla akautoa nje na kukata kata nikiwa namwona mimi nilichofanya nikaenda mkatia RB ninayo mpaka sasa. Sema tu kinachonikwamisha ni hili jeshi letu linao watu wenye tamaa ya fedha ndani yake ndio nahofia kwenda pupa. Ndio maana nikaja hapa jukwaani kama nitaweza pata mtu makini anisaidie huyu kijana awajibishwe kulingana na makosa yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kusoma hadi hapa, naomba nihitimishe kwa kusema kwamba....
Hii ni misuguano/magomvi ya kifamilia, na tukifuatilia sana yawezekana tutagundua kwamba huu ugomvi umerithi kutoka kwa vizazi hata viwili kabla ya ninyi kuzaliwa.

Hivyo..... ebu naomba nishike jembe nikalime mie...
 


Huyo ni ndugu yako wa damu kabisa hiyo rb achana nayo na asijue kama umekata..
Tafuta wakubwa zenu wa familia mshktakie huyo bwana kwa wakubwa zako..mambo yaishe kifamilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…