Wilhelm Johnny
JF-Expert Member
- Jan 13, 2016
- 1,368
- 1,325
Habari za asubuhi wakuu niilikua naomba msaada wa kisheria juu ya uharibifu wa mazao nasema uharibifu wa mazao kwa sababu kama mtu kakuharibia kifaa cha shamba kwa makusudi na kusababisha mazao kukauka si sawa na kuingia shamba kuharibu mazao. na huyu kijana hii nitabia yake kufanya vurugu na kuharibu vitu akipelekwa polisi mama yake hutoa hongo na kesi zinapindishwa. Huyu kijana amekatakata mpira wa mita 50 niliokua natumia kunyeshelea kwenye mboga na mipapai. Mimi nina RB yake hapa wiki ya pili nikipiga mahesabu ya kwenda Polisi nikifikiria na fedha watakazohitaji na hapa sina chochote naishia kukata tamaa kama kuna aliyeko moshi na anauwezo wa kunisaidia jamani naomba msaada wake kisheria huyu kijana aadhibiwe kwa kosa alilofanya maana mtu najitahidi kupambana siibi cha mtu ni jitihada zangu mwenyewe bado kuna kuja mtu anafikiria kukurudisha nyuma. Naambatanisha na picha za eneo la bustani lililoharibiwa na ukame baada ya mpira kukatwa katwa. Nina Ishi Moshi Mjini.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app